Na Gladness Mushi, Arusha
Akitangaza rasmi vita hiyo ambayo itafanyika katika mikoa
yote hapa nchini kaimu Kamishna mkuu wa mamlaka hiyo Rishedi Bade
alisema kuwa serikali kamwe haitaweza kuwafumbia macho wadanganyifu wa
biashara ya aina yoyote ile
MAMLAKA ya mapato TRA hapa nchini imetangaza vita kubwa kwa
wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambao wanashinikiza mgomo wa kufunga
biashara kwenye maduka mbalimbali hapa nchini kwa visingizio vya
kutotambua matumizi ya mashine za kulipia kodi
Aidha hatua hiyo inakuja wakati wafanyabiashara katika mikoa
mbalimbali hapa nchini kufunga maduka na kisha kushinikiza kwa wenzao
wasitoe huduma kwa ajili ya kupinga matumizi ya mashine hizo
Katika hatua nyingine alisema kuwa
matumizi ya mashine hizo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa la
Tanzania kwani zinaweka na kuanisha wazi juu ya mapato halisi ya
mfanyabiashara
0 comments:
Post a Comment