
Ndugu zangu,
Kwa akili ya kawaida kabisa, mwanadamu
unaweza kupata tabu kuamini kuwa TUME ile ya Warioba iliyoundwa na
wateule wa Rais wakiwemo wasomi mahiri, majaji na maprofesa, ikatoka na
mapendekezo ya Kijinga-jinga kama hili la Muundo wa Serikali Tatu kama
wengine wanavyotaka tuamini.
Nimepata kusema, kuwa haiyumkini
Majaji wetu hawa wazaliwa na wazalendo wa nchi hii wakawa wote wana
matatizo katika kufikiri kwao; Jaji Francis Nyalali, Jaji Robert
Kissanga, Jaji Joseph Warioba, Jaji Augustine Ramadhan na Jaji Mark
Bomani. Kwamba wote hawa, na katika nyakati tofauti, wamependekeza mfumo
wa Serikali Tatu ili kuunusuru na kuuimarisha Muungano wetu.
Nahofia, kuwa baadhi ya wanasiasa wetu
ndio wenye matatizo katika kufikiri kwao, na pengine wana '
Intellectual arrogance'- Ujivuni wa kiakili.
Na isije ikawa, kuwa wanaangalia
kwanza ni mfumo gani wa Serikali utakaowanufaisha wao binafsi, makundi
yao na vyama vyao kwa kuangalia namna watavyoshinda chaguzi za kisiasa
na kushika madaraka.
Wanaangalia zaidi leo na kesho. Kwao kesho kutwa na mtondogoo ni mbali sana.
Naam, tumwamini nani? Maana, iliimbwa, kuwa ' Mwanasiasa' ni ' kigeugeu! Na Jaji naye....?
Habari hii imendikwa na Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.
0754 678 252
0 comments:
Post a Comment