Christiano Ronaldo jana aliiwezesha
timu yake ya Real Madrid kutinga katika fainali za kombe la Copa Del Rey
baada ya kuichapa Atletico Madrid katika mtanange wa Madrid derby;
ushindi huo wa magoli 2-0 tayari umeipa timu ya Real Madrid jumla ya
magoli 5-0 dhidi ya maadui zao hao wakubwa (Atletico Madrid) kwa kuwa
katika mchezo ulioshuhudiwa jumaatano ya wiki iliyopita wakati Real
Madrid ilipoitandika Atletico magoli 3-0 katika uwanja wa Sentiago
Bernabeu.
Real Madrid sasa inamsubiri mshindi
kati ya Barcelona au Real Sociedad ili kukutana katika mchezo wa fainali
za kombe hilo zitakazichezwa mwezi Marchi; ikumbukwe kuwa timu ya
Barcelona iliifunga timu ya Real Sociedad magoli 2-0 ikiwa katika uwanja
wake wa nyumbani na timu hizo tinakutana tena leo katika mzunguko wa
pili wa kombe hilo la Copa Del Rey.
Chanzo, goal.com
0 comments:
Post a Comment