Wanafunzi hao wakiwa na mabango mbali mbali leo katika viwanja vya chuo hicho
Polisi wakithibiti maandamano hayo
WAnafunzi hao wakiwa katika viwanja vya chuo hicho leo
Makamu Mkuu wa Chuo, Mlenge |
Rais wa serikali ya wanafunzi, Manfred Joachim |
WANAFUNZI
wa chuo cha ualimu Kleruu kilichopo Gangilonga mjini Iringa, wamefanya
maandamano wakipinga kukosa huduma ya umeme kwa wiki ya tatu sasa baada
ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwakatia.
Maandamano
hayo yaliyoanzia chuoni hapo leo kuelekea ofisini na hatimaye
nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, yalidhibitiwa na Jeshi la Polisi
yakiwa yamekaribi shule ya msingi Um-salam kwa kile kilichoelezwa kwamba
hayakuwa na kibali..
Rais
wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho, Manfred Joachim alisema wametii
amri ya Polisi lakini watayafanya tena Jumatatu baada ya kukamilisha
taratibu zote ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha Polisi.
Joachim alisema wameamua kutumia mbinu hiyo ili kuongeza msukomo kwa uongozi wa chuo na serikali kuitatua kero hiyo.
“Hatuwezi
tena kujisomea usiku na mafunzo ya teknlojia ya habari na mawasiliani
yaani ICT yamesimama; wanafunzi wamekata tamaa, hawajui hatma yao wakati
ada wamelipa,” alisema.
Wakiwa
wamekusanyika katika uwanja wa michezo wa chuo hicho chini ya ulinzi wa
Polisi, kiongozi huyo alisema huduma ya maji nayo ni kero kubwa chuoni
hapo.
“Wakati
mwingine zinaweza kupita zaidi ya siku mbili hatujaoga; yote hayo ni
kwasababu tuaambiwa na uongozi wa chuo kwamba hawana fedha za kulipia
huduma hizo,” alisema.
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Anjelist Mlenga alisema uongozi wa chuo unawaonea
huruma wanafunzi hao lakini akakosoa taratibu wanazozitumia kudai huduma
hizo.
Akiwa
hajui kiasi cha fedha kinachodaiwa kwa ajili ya huduma ya maji, Mlenga
alisema deni la umeme chuoni hapo ni zaidi ya Sh Milioni 2.5.
Alisema Mkuu wa chuo hicho amekwenda wizarani kufuatilia fedha hizo kwakuwa wao ndio wenye jukumu la kulipia huduma hizo.
“Mkuu
wa Chuo yupo wizarani, naomba muwe wavumilivu kwani hata kama
atakubaliwa fedha hizo, kwa taratibu za serikali inaweza kuchukua wiki
nyingine kuzipata,” alisema.
Akizungumzia
ombi la wanafunzi hao la kukifunga chuo hicho mpaka pale huduma hizo
zitakaporejea, Mlenga alisema “ ni jambo linalojadirika, tutaona mpaka
wiki ijayo hali itakavyokuwa na tutaangalia cha kufanya.”
Aliwasihi
wanafunzi hao kuacha kuyachanga madai yao na itikadi zao za kisiasa kwa
kuzingatia kwamba mambo hayo yanapigwa marufuku katika taasisi za
elimu.
0 comments:
Post a Comment