Sunday, 2 February 2014

MWANAMKE AFARIKI KWA KUTEKETEA KWA MOTO DAR.

Mwanamke  anayekadiriwa   kuwa  na  umri  kati   ya   miaka  15  hadi  20 , ambaye   jina  lake  halikuweza  kufahamika  mara  moja  amefariki  dunia  baada  kuungua  na   moto  uliozuka  ghafla  ndani  ya  nyumba.

Taarifa  kutoka  jeshi  la  polisi  kanda  maalum  ya  Dar  es  salaam , zinaarifu  kuwa  tukio  hilo lilitokea  February  mosi  saa  nane  na  nusu  usiku   maeneo  ya  Chanika  Kimwani , ambapo  moto  ulizuka  ghafla  katika  nyumba  ya  Theresia  Pius  (45)   na  kuteketeza  vitu  vyote  vilivyokuwemo  ndani  ya  nyumba  hiyo  pamoja  na  kumuunguza  mwanamke  huyo.

 Aidha  taarifa  zinaeleza   kuwa  mwanamke  huyo  aliyefariki,   enzi  za  uhai  wake  aliachwa  na  mmiliki  wa  nyumba  hiyo  hadi  atakaporejea , hivyo  wakati   tukio  hilo  likitokea  mmiliki  wa  nyumba  hiyo  hakuwepo.
Hata  hivyo   chanzo  cha  kuzuka  kwa  moto  huo  bado  hakijafahamika  na  jitihada  za  kumtafuta  Theresia  Pius  ili  kupata  taarifa  zaidi  zinaendelea.
Sambamba  na  hayo , hakuna  mtu  aliyekamatwa  juu  ya   tukio  hilo  na  maiti  imehifadhiwa  hospitali  ya  Taifa  muhimbili   huku  upelezi  ukiendelea.  

Na Kenneth John wa  , Dar-es-salaam

Related Posts:

0 comments: