Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi
alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi
kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo
hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
Masimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid ,
akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika kwa kazi ya uhesabuji wa
Kura na kuzijumlisha kura zote zilizopingwa na Wananchi wa Jimbo hilo.
Akitangazo matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki
yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake.
Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama
cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa Kura 1856, sawa
na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo
hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid,
aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi
kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho.
Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445,
sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid
amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa
na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza
tangu kuazishwa kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika
jimbo la Chambani,Pemba.
Nae Mgombea wa Chama cha CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34
sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la
kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6
sawa na asilimia 0.3. Nae Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai
Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1
Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama
cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi
Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya
ushindi huo.
0 comments:
Post a Comment