Na Kenneth John Dar
Mwanaume mmoja
aliyefahamika kwa jina
la Masoud Jaffar
(30) ambaye kazi
yake ni kuchimba
mashimo, amefariki dunia
baada ya kuangukiwa
na kifusi.
Taarifa kutoka
jeshi la polisi
kanda maalum ya
Dar es salaam
zinasema kuwa, February
3 majira ya saa
kumi na mbili
na dakika ishirini
jioni huko
barabara ya Mandela ,
eneo la kurasini
Baraza la maaskofu , mtoa taarifa
Said Ally Nayeka (35) ambaye
ni mkazi wa
Buza kwa lulenge
na pia ni
Operator Ravji
Construction Ltd alilieleza jeshi
la polisi kuwa
akiwa na wenzake
mara baada ya
kumaliza shughuli ya
kutoboa mashimo ya
kupitishia bomba za gesi
chini ya barabara
ya Mandela, kwa
bahati mbaya walisahau
mkasi,kisu na mashine
ya kutoboa ardhi
ndani ya mashimo
hayo waliyokuwa wakichimba
na ndipo Masoud
Jaffar aliingia ndani ya
shimo ili kutoa
vitu hivyo.
Na akiwa
bado ndani ya
shimo ghafla aliangukiwa
na kifusi cha
mchanga na kufunikwa
na hatimaye alifariki
dunia papo hapo.
Aidha taarifa
zinaendelea kusema kuwa
kifusi hicho kilianguka
baada ya mtikisiko
wa lori lililopita
karibu na shimo
hilo ambalo namba
zake hazikufahamika .
Maiti ilifukuliwa
na mwili wake
umehifadhiwa hospitali ya
Temeke huku upelelezi
ukiendelea.
Na katika
tukio lingine lililotokea
maeneo ya Boko
beach wilaya ya
kinondoni, imekutwa maiti
ya mtoto mchanga
anayekadiriwa kuwa na
umri wa siku 1
.
Ambapo kwa
mujibu wa jeshi
la polisi kanda
maalum ya Dar es
salaam maiti ya
mtoto huyo mchanga
ilikutwa ikiwa imeviringishwa nguo
na mtu asiyefahamika .
Maiti imehifadhiwa
hospitali ya Mwananyamala
na hakuna aliyekamatwa ,upelelezi unaendelea.
0 comments:
Post a Comment