TRA WASEMA WAHAJAMNYANYSA MFANYABIASHARA YETOTE
Meneja wa TRA Iringa |
WAFANYABIASHARA
mkoani Iringa wafanya mgomo baridi wa kufungua maduka yao huku
wakipita mitaani kuwafanyia vurugu wenzao wanaogoma kufunga maduka yao kama sehemu ya hatua ya kuishinikiza serikali kuachana na kuwalazimisha kununua mashine za kodi za kielektroniki (EFD)
Hatua
hiyo imepelekea serikali mkoa wa Iringa ikitoa onyo kali kwa kikundi
cha wafanyabiashara wanaowafanyia fujo wengine na kuliagiza jeshi la
polisi kuwakamata .
Akizungumza
na wanahabari ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine
Ishengoma alisema wamepata taarifa ya kuwepo kwa kikundi cha watu
wachache ambao wanawafanyia vurugu wenzao ambao wanataka kufungua
maduka hayo na tayari msako mkali umeanza toka leo ili kuwakamata
watu hao.
“
mimi ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama pia mkoa hivyo
sitapenda kuona amani inavurugwa na wachache ….pia tutambue wapo
wenye mikopo; kwa faida yao, ya jamii na kwa maendeleo ya mkoa wa
Iringa naomba warudi kwenye biashara wakati serikali ikichukua kilio
chao na kukifanyia kazi,” alisema.
Taarifa za
wafanyabishara hao ya kufunga maduka yao mpaka pale serikali
itakapositisha matumizi ya mashine hizo, ilianza kuenea jana kwa kupitia
mitandao ya simu na taarifa kutoka kwa kikundi kinachoendesha kampeni
hiyo.
Biashara pekee zilizokuwa zikiendelea kwa jana ni zile za vyakula katika masoko mbalimbali ya mjini Iringa.
Huku
maduka ya nguo nay ale ya vifaa mbali mbali yalionekana kufungwa huku
bar na maeneo ya soko na vyakula ndio yalionekana kufanya kazi .
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa
Iringa, Lucas Mwakabungu alisema wamepanga kukutana na wafanyabiashara
hao saa tisa mchana wa huu ili kuwashauri wasiendelee na mgomo.
“Tunachukua
kero yao na tunawaahidi tutakaa meza ya pamoja na serikali ili tufikie
muafaka; mfanyabishara nayajua umuhimu wa mzunguko wa fedha yake
hatakiwa kupoteza mapato kwa migomo kama hii,” alisema.
Hata
hivyo alisema kuwa mgomo huo ni batili kwani hauna baraka za
TCCIA mkoa wa Iringa na kuungana na serikali ya mkoa kutaka
wahusika wa mgomo huo kusakwa .
Wakizungumzia
mgomo huo wafanyabiashara Sara Sanga na Boniface Bukuku walisema wao
ni mmoja wa wafanyabishara wa vitu vya urembo pia wanatakiwa kununua
mashine hizo.
Alisema
Bukuku kuwa kwa mwaka amekadiriwa kulipa kodi ya Sh 574,000 kwa mwaka
akiweka na mashine hiyo atalazimika kulipa fedha nyingi zaidi TRA,”
alisema.
Akitoa
mfano alisema kama mapato yake kwa mwezi ni Sh Milioni 2, atatakiwa
kulipa wastani wa Sh200,000 kila mwezi kama kodi ya ongezeko la thamani
(VAT).
“Kwahiyo
kwa mwaka nitatakiwa kulipa Sh Milioni 2.4 pamoja na makadiro ya kodi ya
Sh 574,000, jumla natakiwa kulipa kiasi kinachokaribia Sh Milioni 3,”
alisema.
Alisema kiasi hicho cha kodi ni nje ya kodi ya pango, mishahara ya wafanyakazi na huduma zingine za uendeshaji.
Huku Bi
sanga akiadai kuwa TRA mkoa wa Iringa imekuwa ikiwanyanyasa kwa
kuwataka kununua mashine hiyo na kuwa wameamua kufunga kutokana na
kubanwa kununua mashine hizo bila ya kuwa na elimu ya matumizi yake.
Mbali ya
idadi kubwa ya wafanyabiashara kugoma ila baadhi yao walidai kuwa
wanalazimishwa kugoma japo wapo tayhari wamenunua mashine hizo na
kuiomba serikali kuwawekea ulinzi ili leo waweze kufungua maduka yao .
Meneja wa TRA mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda alisema
kuwa ofisi yake imeendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu kupitia semina mbali mbali na kamwe
haijapata kuwanyanyasa wafanyabiashara hao.
Hata
hivyo alisema kuwa hakuna atakayewafungia biashara kwa sasa bila
ya kuwaandikia barua na kuwataka wafanyabiashara hao kwa wale wasio
na elimu ya mashine hizo kufika ofisini kwake .
0 comments:
Post a Comment