Godfrey Mgimwa |
Katika pingamizi lao lilowasilishwa juzi, Chadema walikuwa wanapinga Godfrey Mgimwa kugombea ubunge kupitia CCM kama alivyoomba kwa kuwa sio raia wa Tanzania.
Tetesi za tatizo la uraia wa Godfrey Mgimwa zilisambaa mjini Iringa baada ya Chadema kuweka pingamizi hilo.
Katika Pingamizi lao hilo, Chadema ambao katika uchaguzi huo mdogo wamemsimamisha Grace Tendega kupeperusha bendera yao walisema Godfrey Mgimwa anakosa sifa ya kuwamgombea wa chama chochote cha siasa nchini kwa kuwa aliukana uraia wake.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisika hakuweza kupatikana jana, lakini Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga alithibitisha pingamizi hilo kutupiliwa mbali.
"Ulikuwa ni uzushi dhidi ya mgombea wetu, hatukuwa na hofu yoyote kwakuwa mgombea wetu anakidhi sifa zote," alisema.
Alisema Chadema wameshindwa kuwasilisha ushahidi unaonesha Godfrey Mgimwa aliukana uraia wa Tanzania alipokuwa masomoni nchini Uingereza.
Baada ya kushindwa kuwasilishwa ushahidi wowote, madai hayo yamedhihirika kwamba ni ya uongo na msimamizi wa uchaguzi ametupilia mbali pingamizi hilo hivyo Mgimwa ni mgombea halali wa CCM katika uchaguzi huo.
Katibu wa Chadema Iringa Vijijini Felix Nyondo hakupatikana kuzungumzia pingamizi lao kutupwa na hata alipokuwa akitafutwa kwa simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.
Mtenga alisema kesho atakutana na wanahabari ili kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maandalizi ya kampeni za uchaguzi huo.
Kampeni za uchaguzi huo zilianza februari 19 na zinatarajia kukoma Machi 15 ambayo ni siku moja kabla ya Uchaguzi huo wa Machi 16.
0 comments:
Post a Comment