>>JUMAPILI: ATLETICO AU REAL KUTWAA UONGOZI?!
LA LIGA sasa ni mshikemshike kweli baada
ya Leo Valencia kufanya kweli Uwanjani Nou Camp na kuichapa Barcelona
Bao 3-2 na kuwaweka Mabingwa hao kwenye njia panda maana Jumapili
Atletico Madrid au Real Madrid zina nafasi kubwa kuwapiku uongozi wa
Ligi.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | FC Barcelona | 22 | 17 | 3 | 2 | 59 | 16 | 43 | 54 |
2 | Atletico de Madrid | 21 | 17 | 3 | 1 | 52 | 14 | 38 | 54 |
3 | Real Madrid CF | 21 | 17 | 2 | 2 | 60 | 21 | 39 | 53 |
4 | Athletic de Bilbao | 21 | 13 | 3 | 5 | 41 | 27 | 14 | 42 |
Barca
walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 7 Mfungaji akiwa Alexis
Sanchez na Valencia kujibu na kupiga Bao mbili katika Dakika ya 44
lililofungwa na Parejo na Dakika 4 baadae kupitia Pablo Piatti.
Barca walisawazisha kwa Penati ya Lionel
Messi na hilo ni Bao lake la kwanza baada kutofunga katika Mechi 3
lakini Paco Alcácer, katika Dakika ya 59, aliipigia Valencia Bao la 3 na
kuwapa ushindi.
Barca walimaliza wakiwa Mtu 10 baada
Jordi Alba kupewa Kadi ya Njano ya pili kwenye Dakika ya 78 na kutolewa
nje kwa Kadi Nyekundu.
Ukiiondoa Real Madrid, Valencia imekuwa
Timu ya kwanza kuondoka Nou Camp bila kufungwa tangu Oktoba 2011 Sevilla
ilipopata Sare ya 0-0.
Matokeo haya yameiacha Barca uongozini
ikiwa Pointi 54, sawa na Atletico Madrid, lakini Atletico wana Mechi
moja mkononi ambayo watacheza Nyumbani kesho Jumapili na Real Sociedad
wakati Real Madrid, walio Pointi 1 nyuma ya Barca na Atletico, pia
watacheza Jumapili Ugenini na Athletic Bilbao.
Atletico na Real zina nafasi nzuri kuitungua Barca toka kileleni.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Ijumaa Januari 31
Granada CF 1 Celta de Vigo 2
Jumamosi Februari 1
FC Barcelona 2 Valencia 3
Levante v Rayo Vallecano
Getafe CF v Real Valladolid
Malaga CF v Sevilla FC
Jumapili Februari 2
Elche CF v UD Almeria
Real Betis v RCD Espanyol
Atletico de Madrid v Real Sociedad
Athletic de Bilbao v Real Madrid CF
Jumatatu Februari 3
Villarreal CF v Osasuna
0 comments:
Post a Comment