MCHEZAJI MPYA wa Arsenal, Kim Kallstrom, atakuwa nje kwa muda baada kugundulika ameumia Mgongo.
Kallstrom, Miaka 31, inadaiwa aliumia
Mazoezini Jumanne huko Abu Dhabi, UAE, wakati alipokuwa na Klabu yake
Spartak Moscow na aliwaeleza Arsenal matatizo yake hapo Jana alipotua
London kwa upimwaji Afya lakini Vipimo vya MRI havikuonyesha tatizo
lakini Kipimo cha CT kilionyesha lipo tatizo kwenye Mgongo wake.
Inadaiwa Wenger alijulishwa taarifa hizi
lakini ikaamuliwa wakamilishe Usajili wake hiyo Jana ambayo ndio
ilikuwa Siku ya mwisho ya Uhamisho wa Wachezaji kwenye Dirisha la
Uhamisho la Januari.
Inakisiwa Kallstrom atazikosa Mechi 6 za
Arsenal ambazo ni dhidi ya Crystal Palace, Liverpool, mara mbili,
Manchester United, Bayern Munich na Sunderland.
Kallstrom, Raia wa Sweden aliewahi kuichezea Lyon ya France, ndie Mchezaji pekee
aliesainiwa na Arsenal kwenye Dirisha la
Uhamisho la Januari na amesainiwa kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu ili
kuziba pengo la Viungo Majeruhi Aaron Ramsey na Jack Wilshere pamoja na
Mathieu Flamini ambae amefungiwa Mechi 3 baada Kadi Nyekundu.
Mchezaji huyo sasa anatarajiwa kurudi
kwao Sweden kisha kwenda Urusi na baadae kurudi London kuendelea na
Matibabu akiwa na Arsenal.
0 comments:
Post a Comment