Thursday, 13 February 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 RAIA WA NCHINI KONGO BAADA YA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI .

DSC00207
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 WOTE RAIA NA WAKAZI WA SANGE – BUKAVU NCHINI KONGO WAKIONGOZWA NA HESABU LUHIGITA (16) BAADA YA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IKUMBILO WILAYA YA ILEJE WAKIWA WANASAFIRISHWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.136 AQC AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MUSSA DISI (35) NA MATEO KADUMA (30)  WOTE WAKAZI WA ISONGOLE AMBAO PIA WAMEKAMATWA PAMOJA NA GARI HILO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA  KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Related Posts:

0 comments: