Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro |
MWANDISHI WILLIAM BUNDALA KANDA YA ZIWA
Tukio hilo limetokea jana Majira ya saa moja jioni wakati wafuasi hao wa CCM wakitoka
katika mkutano wa Hadhara wa kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Ubagwe wilayani Kahama....
katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa kabisa mkono wake wa kushoto |
Waliojeruhuwa
katika tukio hilo ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud
Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na Afisa mtendaji
kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro ambaye amekatwa panga usoni.
Wengine
ni katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga
ambaye amekatwa panga kichwani na kukatwa kabisa mkono wake wa
kushoto na dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa
mapanga Kichwani.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono |
Pia
amejeruhiwa Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha
Mapinduzi aliyejeruhiwa mguuni pamoja na Subira Nyangusu, huku ikielezwa
kuwa watuhumiwa wa tukio hilo walipasua vioo vya gari la CCM na
kuchukua funguo za gari hiyo.
Kwa
mujibu wa Mganga Mkuu wilaya ya Kahama, Andrew Emanuel majeruhi hao
wamelazwa katika hospital ya wilaya hiyo, huku Kimaro, Masunga na Peter
ambao hali zao ni mbaya wakipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini
Mwanza.
Dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani. |
Imedaiwa
katika tukio hilo wafuasi hao wa Chadema wamepora fedha zaidi ya
shilingi milioni moja na laki tatu kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na
simu za mkononi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amesema watuhumiwa 16 wa tukio hilo ambao ni wafuasi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilaya ya Kahama.
Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama |
0 comments:
Post a Comment