KOCHA
wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kwamba Cristiano Ronaldo
amepona tena baada ya kuumia maumivu ya nyama katika mchezo dhidi ya
Valladolid.
Mreno
huyo alilazimika kutoka nje Madrid ikilazimishwa safe ya 1-1 katika
mechi ya La Liga na akakosa mchezoa ambao timu yake hiyo ilifungwa 2-0
na Celta Vigo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Lakini
akizungumza kuelekea mchezo wa leo na Espanyol, Ancelotti alisema
kwamba nyota wake huyo atacheza katika sehemu fulani ya mchezo huo wa
mwisho wa msimu wa nyumbani.
Habari
zitakuwa ahueni kubwa kwa mashabiki wa Los Blancos, ambao tayari
wanautazama mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi ijayo
dhidi ya wapinzani wao wa nyumbaniu, Atletico Madrid baada ya kutupwa
nje ya mbio za ubingwa wa Hispania.
Xabi
Alonso ataukosa mchezo wa Lisbon baada ya kupewa kadi ya nano katika
Nusu Fainali Real wakiifunga Bayern Munich, lakini Ancelotti
anafurahishwa na viungo wa kati waliopo.
Amesema:
"(Asier) Illarramendi ni suluhisho la kwanza, kwa sababu tulimsajili
kuchukua nafasi ya Xabi (Alonso) na anajua namna ya kucheza katika
nafasi hii. Illarra ana ubora wa kutosha kucheza katika mechi zote, muhimu ni kwamba tunafurahi kuwa naye,".
Maandalizi: Wachezaji wa Real wanakabiliwa na fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani, Atletico Madrid
Sami Khedira yuko pia kwenye nafasi ya kuziba pebgo la Alonso baada ya kupona maumivu yake ya muds mrefu ya goto na Ancelotti amesema kwamba Mjerumani huyo atacheza dhidi ya Espanyol.
"Khedira
atapewa dakika kadhaa kesho (leo) kwa sababu anahitaji kucheza.
Alkifanya vizuri dhidi ya Celta Vigo,"alisema. "Anaweza kuwa sukuhisho
kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa,".
0 comments:
Post a Comment