MSHAMBULIAJI Luis Suarez amesema anapenda maisha ndani ya Liverpool na hafikirii kuondoka Anfield.
Nyota
huyo wa Uruguay amemaliza msimu vizuri akiwa na Wekundu hap kwa kufunga
mabao 31 na kutwaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha Wachezaji wa
Kulipwa (PFA) na ya Waandishi wa Habari za Soka.
Mafanikio
hayo yanakuja baada ya kupitia msimu mgumu uliopita akifungiwa kwa
kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic - akilazimisha kupita.
Siondoki:
Mshambuliaji Luis Suarez amesema hana mpango wa kuondoka Liverpool
licha ya kutakiwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona
Sasa
wakati tetesi za usajili zimeanza tena, Suarez, ambaye mapema wiki hii
alikanusha kuwa na nia ya kuhamia klabu nyingine kubwa Ulaya, ameamua
kuuheshimu mkataba aliosaini Desemba mwaka jana.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ameripotiwa kutakiwa na Real
Madrid, ameiambia Sky Sports kwamba: "Nilisaini mkataba kwa sababu
napapenda haps na nina furaha dana hapa. Ikiwa haunt furaha hapa huwezi
kusaini mkataba wowote,".
"Liverpool
kwangu ni moja ya timu bora duniani, kwa sababu hakuna mtu haps katika
chumba cha kubadilishia nguo anafikiri mimi no bora zaidi ya wengine na
watu hapa ndani ya Melwood wanafanya kazi vizuri,"alisema.
0 comments:
Post a Comment