Wanafunzi waliodaiwa kunusurika kusafirishwa hawa hapa
..............................................................................
HUKU mkoa wa Iringa ukiwa katika vita
vikali vya kuwalinda watoto wa kike kutoka mkoani hapa kwenda
mijini kufanyishwa kazi za ndani (uyaya) na katika madangulo ,watoto wa
kike wameendelea kugeuka dili kubwa mkoani Iringa baada ya mwamake
mwingine mjini hapa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusafirisha
watoto wa kike sita kwenda kuuzwa kwa ajili ya kufanya kazi za ndani
mijini
Kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa
mwanamke huyo kunaendelea kutishia usalama wa watoto wa kike katika
mkoa wa Iringa kutokana na wimbi hilo la usafirishaji watoto wa kike
kwenda mijini baada ya mwezi huu mmoja kukamatwa wanawake wawili kwa
kujihusisha na biashara hiyo ya watu.
Mwanamke wa kwanza alikamatwa eneo la
Frelimo akitaka kumtorosha mfanyakazi wa ndani na kuishia kupewa
kichapo kama adhabu yake ya kufanya biashara hiyo ya watu .
Wakati tukio jingine ambalo linafanana
na hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii baada ya mwanamke mmoja Bi
Amina Sanga (42) ambae ni mke wa aliyepata kuwa mfanyabiashara
maarufu mjini hapa kujikuta akifikishwa mahakamani kwa tuhuma za
kutaka kuwasafirisha watoto sita wa kike kwa ajili ya kwenda
kufanyakazi za ndani mijini.
Mwanamke huyo ambae alifikishwa siku
ya jumanne wiki hii mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo Bomani
mheshimiwa Alois Masua alipata kusomewa shitaka hilo la jinai namba
33 la mwaka huu .
Akisoma shitaka hilo hakimu Masua
alisema kuwa mwanamke huyo mkazi wa Mgela Iringa vijijini
anatuhumiwa kwa kosa la kusafirisha watoto sita wa kike ambao ni
wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Mgela.
Kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa majira
ya saa 10 alfajiri ya mwishoni mwa wiki kutokana na mtego uliowekwa
na wananchi wa eneo hilo.
Katika kesi hiyo mlalamikaji ni mtoto
Sophia Kitule kwa niaba ya wenzake watano ,mshitakiwa alikana
shitaka hilo na mahakama hiyo kudai kuwa dhamana yake ya kuwa na
wadhamini wawili kila mmoja akiwa na barua ya dhamana ya Tsh milioni 1
na mali isiyohamishika .
Hata hivyo mshitakiwa huyo
alilazimika kwenda mahabusu hadi tarehe 12 ya mwezi ujao baada ya
wadhamini wao kukosa sifu baada ya kufika mahakamani hapo wakiwa
mikono mitupu bila barua .
0 comments:
Post a Comment