Tanga. Uvutaji wa sigara umeleta maafa, baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea sigara.
Katika tukio hilo lililotokea Korogwe, Jumapili iliyopita, Februari
2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa miaka 30 alimkata
mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea ugomvi uliohusu
sigara.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Massawe alisema kuwa
Polisi Tanga wako katika msako mkali wa kumtia nguvuni Iddi Mkono (30)
kwa tuhuma za mauaji.
Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.
Wakati huo huo, watu wawili wanashikiliwa na polisi, mkoani hapa kwa
tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu ya gongo maeneo ya
Handeni, mkoani Tanga.
Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.
Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.
Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua tahadhari na
matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza kusababisha kuvunja
sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria zilizowekwa
atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment