Thursday, 16 January 2014

XAVI LEO KUFIKISHA MECHI 700 NA BARCA;; NI REKODI KWA BARCA!

XAVI_wa_LEO_JANAXAVI, Kiungo wa Barcelona ambae atatimiza Miaka 34 baadae Mwezi huu na ambae ndie ameichezea Klabu hiyo Mechi nyingi kupita yeyoye, Usiku huu anatarajiwa kucheza Mechi yake ya 700 wakati watakapokuwa Ugenini kurudiana na Getafe kwenye Mechi ya Copa del Rey.
Xavi, ambae alianza kuichezea Barca Mwaka 1998, alivunja Rekodi ya kuichezea Mechi nyingi Mwaka 2011 alipoipiku Rekodi ya Beki wao wa zamani Miguel aliecheza Mechi 549.
Anaefuatia kwa Mechi nyingi ni Nahodha wa sasa Carles Puyol ambae Usiku huu atafikisha Mechi yake ya 589 kwa Barca.
Xavi alianza kuchezeshwa chini ya Kocha Louis van Gaal na Mwaka huo huo kutwaa Ubingwa wa La Liga na yeye kutunukiwa Tuzo ya Mchezaji Mpya Bora wa Mwaka.
Xavi, ambae ameshatwaa Ubingwa wa Dunia mara moja na Ubingwa wa Ulaya mara mbili akiwa na Spain, ndie Mchezaji pekee wa Barcelona alietwaa Mataji mengi kwa kuzoa Makombe 22.
COPA del REY
Raundi ya Mtoano ya Timu 16-Marudiano
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumanne Januari 14
[Kwenye Mabano Matokeo baada Mechi mbili]
UD Almeria 0 Real Racing Santander 2 [1-3]
Atletico de Madrid 2 Valencia 0 [3-1]
Jumatano Januari 15
Athletic de Bilbao 2 Real Betis 0 [2-1]
RCD Espanyol 4 Alcorcon 2 [4-3]
Osasuna 0 Real Madrid CF 2 [0-4]
Levante 1 Rayo Vallecano 0 [1-0]
Alhamisi Januari 16
22:00 Villarreal CF v Real Sociedad [0-0]
24:00  Getafe CF v FC Barcelona [0-4]
Robo Fainali
Mechi ya Kwanza Jan 21-23, Marudiano Jan 28-30
A RCD Espanyol v Real Madrid
B Levante v Getafe CF/FC Barcelona
C Villarreal CF/Real Sociedad v Real Racing Santander
D Atlético de Madrid v Athletic de Bilbao
Nusu Fainali
Mechi ya Kwanza Feb 5-6, Marudiano Feb 12-13
Mshindi Mechi B v Mshindi Mechi C
Mshindi Mechi A v Mshindi Mechi D
Nusu Fainali
Mechi ya Kwanza Feb 5-6, Marudiano Feb 12-13
Fainali
Aprili 19

0 comments: