HOME »
» WASEMAVYO WANA JIMBO LA KALENGA JUU YA KIFO CHA DR MGIMWA
|
Bw Mario Kihongo katibu uchumi ,mipango na fedha (CCM) kata ya Maboga
Mheshimiwa Mbunge Dr Wiliam Mgimwa
enzi za uhai wake alikuwa karibu sana na wananchi na hata maisha
aliyopata kuishi ni tofauti na viongozi wengine katika serikali
hii ya rais Jakaya Kikwete.
"Natambua ni mapenzi ya Mungu ila
kweli tulimpenda sana mbunge wetu alikuwa ni mtu wa kujishusha
asiyependa kujilimbikizia mali zaidi ya kuwatumikia wananchi
....kweli kifo chake ni pigo kubwa na hatujui kama tutakuja kumpata
kiongozi anayefanana na Dr Mgimwa katika jimbo la kalenga"
Alikuwa ni kiongozi wa kushirikiana
vema na wananchi wake katika shida na raha mfano kata yetu ya
Maboga mheshimiwa Dr Mgimwa ametusaidia mnala wa simu kata ya Maboga
na alikuwa si wa kujisikia kweli kifo chake kimetugusa sana kweli
hatuna la kusema ni Mungu ndie anajua .
Hata hivyo alisema ni pengo kubwa
ambalo wamelipata na hadi sasa hawajui ni nani wa kuliziba pengo
hilo na jimbo hilo la kalenga limepata kuwa na wabunge zaidi ya
watatu ila ni yeye pekee ndie aliyepata kutengeneza miundo mbinu
katika maeneo mengi ya jimbo.
Katika uadilifu kweli ushahidi upo
wazi kutokana na mazingira ya nyumbani kwake Magunga ambapo nyumba
yake ni ya kawaida sana ukilinganisha na nyumba za wananchi wa kawaida
na ni vigumu kuamini kama hapa ndipo nyumbani kwa waziri wa fedha ama
mbunge kwani alikuwa mwadilifu kama hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius
K. Nyerere kwa kuwajali wananchi kwanza kuliko yeye na familia
yake.
|
|
Dismas Mbwela binam wa Dr Mgimwa
.................................................................................................................... Dr Mgimwa alikuwa ni mtu wa maendeleo
na alikuwa habagui na kitu akisema alikuwa akikitekeleza na pale
inaposhindikana alikuwa akirudi na kutueleza ukweli kuwa imeshindikana
na kutoa sababu za kushindikana tofauti na viongozi wengine
ambao hupenda kusema uongo hata pale inaposhindikana kutimiza ahadi
zao
Kweli katika familia yetu alikuwa ni
mlezi wa kweli asiyembagua mtu na siku zote alikuwa ni mshauri wa
familia na hata akirejea kutoka bungeni alikuwa akiishi kijijini
tofauti na wabunge wengine ambao wamekuwa wakiishi mbali na wapiga
kura wao.
|
|
Bw Martine Simangwa aliyekuwa katibu wa mbunge Dr Wiliam Mgimwa .
...............................................................
Aliyekuwa katibu wa mbunge Dr Mgimwa
Martine Simangwa alisema kuwa katika uhai wake mbunge huyo alikuwa
akitaraji kuanza kutimiza ahadi zake ambazo alipata kuwaahidi
wananchi hasa ile ya kusambaza mabati katika shule za msingi na
sekondari.
Simangwa alisema walitegemea kugawa
bati zaidi ya 1170 katika shule na idara ya afya na kuwa bati
hizo alipanga kuzifanya ndani ya wiki mbili zijazo na siku zote
alisisitiza kuwa lazima atimizi ahadi hiyo ya mabati .
" Mimi kama katibu wake na niliyefanya
nae kazi kwa karibu zaidi nitaendelea kukumbatia urithi pekee
alioniachia mimi na wana Kalenga ambapo mara kwa mara alisema kuwa
ili nchi na wananchi waweze kusonga mbele katika uchumi ni lazima
kupata elimu bora na kujiendeleza kwa elimu "
Alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo
alijipanga kuyamalizia kutekeleza kabla ya mwakani wakati wa
uchaguzi mkuu ni pamoja na kuendelea kumalizia viporo vya ahadi
zake katika sekta ya elimu, afya , miundo mbinu na baadhi ya maeneo
kutatua kero ya maji na kila wakati hata akiwa Afrika ya kusini
katika matibabu pindi wanapofanya mawasiliano alikuwa ni mtu mwenye
kupenda kurejea ili kuendelea na ziara ya kutekeleza ahadi zake kwa
wananchi wa jimbo la Kalenga.
TANZIA
WAKUU
WA IDARA/VITENGO
WATUMISHI
WOTE
WIZARA
YA FEDHA
TUNASIKITIKA KUTANGAZA
KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA MHE. DKT.
WILLIAM A. MGIMWA (MB) KILICHOTOKEA TAREHE 01 JANUARI, 2014 HUKO AFRIKA
KUSINI, KATIKA HOSPITALI YA KLOOF MEDI – CLINIC, PRETORIA.
MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 04/01/2014 NA UTASAFIRISHWA KWENDA
MKOANI IRINGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 05/01/2014
KWA MAZISHI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
2
JANUARI, 2014
OFISI
YA WAZIRI MKUU
RATIBA
YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA
DKT.
WILLIAM A. MGIMWA
TAREHE
|
SIKU
|
MUDA
|
TUKIO
|
WAHUSIKA
|
4.1.2014
|
JUMAMOSI
|
7.00 MCHANA
|
MWILI WA MAREHEMU
KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE – TERMINAL II NA KUPELEKWA
NYUMBANI MIKOCHENI B
|
NDUGU
VIONGOZI
WANANCHI
KAMATI
|
11.00 JIONI
|
MWILI KUPELEKWA
HOSPITALI YA LUGALO
|
KAMATI
|
5.1.2014
|
JUMAPILI
|
3.00 – 4.00 ASUBUHI
|
CHAKULA NYUMBANI KWA
MAREHEMU
|
KAMATI
|
4.30 ASUBUHI
|
MWILI KUWASILI
NYUMBANI
|
KAMATI
|
5.30 – 8.00 MCHANA
|
MWILI KUPELEKWA
UKUMBI WA KARIMJEE, KWA AJILI YA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO
|
KAMATI
|
8.00 MCHANA
|
MWILI KUPELEKWA
UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE – TERMINAL 1
|
KAMATI YA KI - TAIFA
|
10.00 JIONI
|
MWILI KUWASILI IRINGA
(NDULI AIRPORT)
NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO - IRINGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
11.30 JIONI
|
KUELEKEA KIJIJINI
MAGUNGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
6.1.2014
|
JUMATATU
|
6.00 MCHANA
|
SHUGHULI ZA MAZISHI
KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA
|
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
|
|
0 comments:
Post a Comment