KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Mechi
hiyo itachezwa Jumamosi Mei 24 mwaka huu katika Jiji la Kaduna kwenye
Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo
unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Ngorongoro
Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza
iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
Mwamuzi
Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka
Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
![]() |
Kikosi cha Ngorongoro kilichofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza na Nigeria Dar es Salaam |
Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment