Wednesday, 22 January 2014

UHAMISHO WAIVA: MATA AKOSEKANA MAZOEZINI CHELSEA HII LEO!!

>>WASHAURI WAKE WATUA ENGLAND TOKA SPAIN!
>>ANELKA AITAKA FA KUFUTA SHITAKA LA 'QUENELLE'!!
>>EVERTON YATOZWA FAINI KWA KURUBUNI MCHEZAJI!
SOMA ZAIDI:
JUAN_MATAANELKA AITAKA FA KUFUTA SHITAKA LA 'QUENELLE'!!
Nicolas Anelka ameitaka FA kufuta Mashitaka dhidi yake kwa kutumia Saluti yake iitwayo 'quenelle'.
Inaaminika Straika huyo wa zamani wa France anaechezea Klabu ya West Bromwich Albion Nchini England anaweza akafungiwa si chini ya Mechi 5 akipatikana na hatia ya kutumia Saluti hiyo inayodaiwa ni ya Kibaguzi.ANELKA-SALUTE
Akiposti kwenye Kurasa yake ya Mtandao wa Facebook, Anelka amesema: “Nawaomba FA kufuta Mashitaka haya dhidi yangu. Narudia, mie sipingi wala kuchukia Wayahudi na si Mbaguzi.”
Anelka pia ameiponda FA kwa kumtumia Mtaalam ili kuchunguza maana ya Saluti yake aliyoitoa mara baada ya kufunga Bao hapo Desemba 28 WBA walipotoka Sare ya Bao 3-3 na West Ham.
Kwenye Akaunti yake ya Twitter, Anelka aliweka Video ya Roger Cukierman, Mkuu wa Kikundi cha Wayahudi CRIF, Representative Council of French Jewish Institutions, ambayo inafafanua kuhusu Saluti hiyo.
Anelka aliitaka FA kuchukua ushauri wa Roger Cukierman huku akisema: “FA wamemtumia Mtaalam ambae ndie ameamua Sakuti yangu ni Ubaguzi. Lakini ingekuwa haki wangemchukua Mtaalam kutoka France, anaeishi France ambae anajua vizuri ishara yangu. Na nani zaidi ya Bwana Cukierman, Mkuu wa CRIF, ambae ameeleza waziwazi 'quenelle' yangu si Ubaguzi. Pia anaeleza waziwazi ni wakati gani ishara hiyo inaweza kuwa ya Kibaguzi.”
FA ilimpa Anelka hadi Alhamisi Januari 23 Saa 3 Usiku kujibu Shitaka lake baada ya kumkabidhi Kabrasha la Kurasa 34 za Tuhuma dhidi yake.
UHAMISHO WA JUAN MATA: WASHAURI WAKE WATINGA ENGLAND TOKA SPAIN!
Wakati Juan Mata hakuonekana kwenye Mazoezi ya Klabu yake Chelsea hii leo huku ikiripotiwa kuwa Mazungumzo ya Uhamisho wake kwenda Manchester United yanaendelea vizuri, Washauri wa Mchezaji huyo hii leo wametua England wakitokea Spain.
Mata amelazimika kutaka kuihama Chelsea baada ya kutopangwa kwenye Mechi na mwenyewe akitaka acheze mara kwa mara ili aongeze nafasi yake ya kuchukuliwa kwenye Timu ya Taifa ya Spain kucheza Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni.
Inasadikiwa Mata atauzwa kwa Dau la Pauni Milioni 37 kwenda Manchester United na hii ni faida kubwa kwa Chelsea kwani walimnunua toka Valencia Mwaka 2011 kwa Pauni Milioni 23.5.
Kwa Misimu miwili iliyopita, Mata, mwenye Miaka 25, ndie alikuwa Mchezaji Bora wa Klabu hiyo kwa mujibu ya Kura za Mashabiki lakini hajaichezea Chelsea tangu Januari Mosi alipobadilishwa kwenye Gemu na Southampton na yeye kupandwa na jazba.
Msimu huu, Mata ameanza Mechi 3 tu kati ya 11 alizoichezea Chelsea kwa vile chaguo la Meneja wao ni kuwachezesha Oscar, Hazard na Willian kwenye Kiungo.
Hadi sasa hamna tamko rasmi toka kwa Chelsea na Man United lakini huko England wanategemea sana Ofa rasmi ya kumnunua itatolewa wakati wowote kuanzia sasa na Mchezaji huyo kufanyiwa upimwaji Afya yake kabla ya Wikiendi hii.
EVERTON YATOZWA FAINI KWA KURUBUNI MCHEZAJI!
Everton imepigwa Faini ya Pauni 45,000 na FA kwa kosa la kumrubuni Mchezaji Chipukizi kujiunga nao kinyume cha Sheria.
Everton walikuwa wakimnyatia Mchezaji wa Timu ya Vijana ya England, Jamaal Lascelles, anaechezea Klabu Nottingham Forest na kosa hilo lilitendeka Mwaka 2010.
Pamoja Faini hiyo, Everton imeonywa ijichunge kuhusu mwenendo wake.
Pia, Wakala aliekuwa akimwakilisha Chipukizi huyo wakati huo, Andy Niedzwiecki, amepigwa Faini Pauni 10,000 na kupewa onyo kali kwa kosa hilo.
Lascelles, ambae sasa ana Miaka 20, ambae amezichezea Timu za Vijana za England za U-18, U-19 na U-20, ameichezea Forest mara 19, mara 15 ikiwa ni Msimu huu, baada kusaini Mkataba wa Miaka minne Mwaka 2012.
Upo wakati Arsenal ilitoa Ofa ya Pauni Milioni 5 kumnunua Kinda huyo lakini Forest iligoma.

Related Posts:

0 comments: