1.UNDP
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Mb akiwa na mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania anayemaliza muda wake Bwana Alberic Kacou  (kushoto) mara baada ya Mwakilishi Mkazi huyo kufika Ofisini kwa Spika  kwa nia ya kumuaga.
 
2.UNDP
Kwaheri na asante kwa kazi nzuri na karibu tena Tanzania ”…. Ndivyo Spika anavyomwambia Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bwana Kacou baada ya kumaliza miaka minne ya utumishi hapa nchini Tanzania.
3.Cuba
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda, Mb, akimkaribisha Balozi mpya wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) ofisi kwake ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kuendeleza ushirikiano wanchi mbili hizi. (Prosper Minja – Bunge).