Duka la Bhangi katika jimbo la Colorado
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa kuvuta Marijuana au Bhangi, sio hatari ikilinganishwa na Pombe.
Lakini Obama amesema kuwa Bhangi bado ni mbaya kwa afya ya binadamu.
Katika mohojiano na jarida la The
New Yorker, alisema kuwa ni vibaya kuwa na dhana kwamba kuhalalisha dawa
hiyo ya kulevya ndio jibu kwa maasi mengi yanayotokea katika jamii
Bwana Obama alikuwa akigusia hatua ya hivi karibuni ya majimbo ya Colorado na Washington kuhalalisha utumiaji wa Bhangi.
Obama aliwahi kukiri kutumia dawa hiyo ya kulevya alipokuwa kijana.
"kama mnavyojua nyote nilivuta Bhangi nilipokuwa kijana na ninaiona kama tabia mbaya sawa na kuvuta sigara,'' alisema Obama
Lakini aliongeza kwamba athari za Bhangi kwa afya ya binadamu sio mbaya ikilinganishwa na Pombe.
Pia alisema kuwa watu masikini wengi wao
wamarekani wenye asili ya kiafrika na walatino, waliadhibiwa visivyo kwa
kutumia Bhangi wakati watu wenye kipato cha kadri walikwepa adhabu
kali.
"ni muhimu kwa jamii kufahamu kuwa sio sawa
ikiwa idadi kubwa ya watu wanovunja sheria hawaadhibiwi vilivyo wakati
wachache wanapata kuadhibiwa.''
Obama alitaja kuhalalisha Bhangi katika majimbo ya Colorado na Washington kama hali ya kutatanisha.
0 comments:
Post a Comment