Mohammed Morsi
Vikosi vya usalama vimeimarisha
ulinzi katika mji mkuu wa Misri Cairo , kabla ya kufikishwa mahakamani
kwa rais aliyeng'olewa madarakani , Mohammed Morsi.
Yeye na maafisa kadhaa wa serikali yake
wanashutumiwa kuchochea ghasia na kuwauwa waandamanaji mwaka 2012 wakati
wa utawala wake. Mashitaka hayo ni pamoja na kushirikiana na wanamgambo
wa kigeni kuvunja gereza.Aling'olewa madarakani kwa mapinduzi mwezi julai mwaka jana na kufungwa . Alipofika mahakamani Mwezi Novemba mwaka jana bwana Morsi alisema kuwa bado yeye ni rais na alifungwa kinyume na matakwa yake
CHANZO BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment