Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi akizungumza na wanahabari leo kuhusu mambo mbali mbali yanayoendelea |
Ofisa habari wa manispaa ya Iringa Sima Bingileki akifuatilia kikao hicho |
HALMASHAURI ya Manispaaa ya Iringa imepiga marufuku ujenzi holela unaoendelea katika milima ndani ya mji wa Iringa .
Kauli hiyo imetolewa leo na mstahiki
meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi wakati
akizungumza na wanahabari ofisini kwake.
Alisema kuwa udhaifu wa usimamizi wa sheria katika maeneo mbali mbali ndio umepelekea ujenzi holela kuendelea.
Hata hivyo alisema nyumba ambazo
zinajengwa kiholela katika mji wa Iringa zitaendelea kuvunjwa iwapo
itabainika kuwa zimejengwa kiholela.
Kuhusu uwekezaji alisema kuwa vipo
viwanja kama vitatu ambavyo vinahitaji uwekezaji na hivyo kuwataka
wananchi kujitokeza kuwekeza katika maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment