Thursday, 23 January 2014

MANCINI AJISIFIA KUHUSU MANCHESTER CITY. ASEMA YEYE NDIYE ALIYEIWEKEA MSINGI BORA


      MANCHESTER CITY
    mancini2_2944041_7676f.jpg
    Aliyekuwa kocha wa timu ya Manchester City ''Roberto Mancini'' ambaye sasa ni kocha timu ya Galatasaray, alitimuliwa na uongozi wa timu ya Manchester City mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka jana,  kocha huyo amesema kuwa yeye ndiye chachu kwa mafanikio ya timu hiyo sasa; alipokuwa na timu hiyo Mancini aliiwezeshatimu hiyo kuchukua kombe la ligikuu ya uingereza na FA hivyo kujiwekea historia yake binafsi ambayo imefufua jina na hata kujulikana kwa timu hiyo ulimwenguni.
    Chini ya uongozi wa Pellegrini, Manchester City tayari inawania mataji manne ya dhahabu na mpaka sasa imeshafikisha idadi ya magoli 106 katika michezo yote waliyoicheza ndani ya msimu huu.(R.M).

    Mancini aliyeitumikia timu ya Manchester City kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu alisema ''nina furaha kwa nilichokifanya Manchester City''.
    Aliendea ''nina furaha kwa kuwa Manchester City ni moja kati ya timu kubwa sana uingereza, na niliijenga vizuri hii timu''.
    Mancini alisema ''nina furahai sana kuwa na hawa wachezaji, nina amani na furaha kubwa katika kazi yangu na pia nina wapenda sana watu wanaoiiendeleza timu hii na nilikuwa na nilipata uzoefu wa kutosha pale''.
    pia alisisitiza kuwa ''Wachezaji wanaofunga magoli wengi ni sehemu ya wachezaji niliowanunua Sergio aguero, Edin Dzeko, Yaya Toure, David Silva na Samir Nasri''.
    ''nadhani Pellegrini anafanya kazi nzuri, lakini nafikiri kuwa wanachokifanya Manchester city tayari tulikifanya miaka mitatu iliyopita, ni sawa tu''. alisema kocha huyo.
    Mancini alitimuliwa mapema tu aliposhindwa kiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya uingereza na pia alipokubali kichapo toka kwa wigani katika fainali za kombe la FA.
    Pia inasemekana kuwa baada ya kushindwa mfulululizo katika michezo hiyo ilidaiwa kuwa meneja huyo hakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya wachezaji katika timu hiyo na hiyo ndiyo sababu kuu iliyomfanya meneja huyo kupoteza kibarua hicho katika timu hiyo.
    Vile vile kocha huyo mwenye asili ya uitaliano alikanusha uvumi kuwa sio kweli kwamba huwa anakosa matumaini katika chumba cha kubadilishia nguo. Alisema '' hayo ni maneno tu, mtu anaweza akatoka nje kuongea tu''.
    ''baada ya miaka minne au mitano kuna uwezekano wa mameneja hao kubadilisha timu''.
    aliongeza ''Nilifanya kazi yangu, vizuri na niliijenga timu nzuri, tulicheza vizuri sana lakini tulishindwa kuchukua ubingwa; hii ni kwa sababu Manchester United walimnunua Van Persie''.
    ''Van persie alikuwa tofauti mwaka jana, nahisi kwa hii miaka mitatu tungekuwa tumebadilisha historia ya Manchester kwa sababu tulicheza mpira mzuri na hadi sasa timu hiyo inafanya hivyo''.
    kocha huyo alisisitiza kuwa ''wakati unafanya kazi unaweza ukapata matatizo na baadhi ya wachezaji, hii ni kawaida kwa kuwa mameneja mda wote hupenda wachezaji kujituma kwa bidii, kucheza vizuri na pia wacheza wanatakiwa wawe waelewa katika hilo''.

    0 comments: