Mwandishi ,Kenneth John wa ,Dar
Tatizo
la foleni za
magari barabarani jijini
Dar es es
salaam ni kikwanzo
kikubwa sana kwa
wakazi waishio jijini
humo kwa muda
mrefu sasa,Na mbaya zaidi foleni
hizo zimekuwa zikikwamisha
shughuli nyingi za
kiuchumi na kibiashara
kwa wakazi wa
jiji hilo na hata kuhatarisha kuvunja
ndoa za watu,
au kuvunja kabisa.Swala
ambalo linachangia kusababisha
uchumi wa mtu
mmoja mmoja na
Taifa kwa ujumla
kuzidi kudidimia siku
hadi siku .
Lakini
serikali imekuwa ikijaribu njia
mbalimbali katika kukabiliana
na tatizo hili, ikiwemo pamoja
na kuweka mataa
sehemu nyingi za
makutano ya barabara
, na
mara nyingine
hata kusambaza askari
wa barabarani sehemu
hizo za makutao
ya barabara hususani
nyakati za asubuhi
na jioni, huku
wakiamini kuwa kwa
kufanya hivyo inaweza
kusaidia kwa kiasi
fulani kupunguza foleni
hizo au hata
kufanya tatizo
hilo kuisha kabisa. Lakini pamoja
na jitihada zote
hizo tatizo hilo
limekuwa likiendelea kukithiri
siku hadi siku.
Na baada ya
jitihada zote hizo
na mbinu mbalimbali
katika kutatua tatizo
la foleni za
magari jijini. Serikali sasa
ikaamua kuja na
njia nyingine mbadala ambayo
inadhaniwa labda itakuwa
ni muarobaini wa
tatizo hilo la
foleni za barabarani na
kufanya kuwa historia.
Mnamo
Septemba 9, 2012 Rais
wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
mheshimwa Jakaya Mrisho
Kikwete aliweka jiwe
la msingi kwenye
kituo kikubwa cha
mabasi ya mradi
wa usafiri wa
haraka Dar es
salaam (DART) Na
kitendo hicho kilidhihirisha kuwa
mpango huo wa
ujenzi wa mabasi yaendayo
kasi umeanza rasmi.
Mradi huo ambao utakuwa na mtandao
wa barabara zenye urefu wa kilomita
137, ambao unajengwa kwa awamu sita hadi
kukamilika kwake, na
taarifa zinasema kuwa mradi utakuwa na njia maalum
ya kupita mabasi
yenye urefu wa kilomita 21, maegesho matatu
ya mabasi (bus
depots) mbili yaani moja Ubungo
na nyingine
Jangwani, vituo vikuu vitano ambavyo
vitakuwa Kivukoni, Kariakoo, Morocco, Ubungo na Kimara, na
vituo vidogo 29 ambavyo
vitajengwa kila baada ya nusu
kilomita.
Mradi unatarajia kukamilika
na kufunguliwa rasmi mwanzoni
mwa mwaka 2015, ambapo inakadiliwa kiasi cha Sh.
bilioni 240.879 kitatumika hadi kakamilika
kwake, ambapo kwa
kukamilika huko watanzania
na wakazi
wa jiji hilo
wanataraji, itakuwa ni
auheni katika shughuli zao
za kila siku, kwani
waliowengi wataanza kufanya
kazi kwa wakati ,
kwani watakuwa wakifika
sehemu zao za
kujipatia mkate wao
wa kila siku mapema zaidi
tofauti na ilivyo
sasa,
Na hii pengine inaweza kuwa chachu ya kuongeza hata vipato vya wakazi wengi wa jiji hili japo kwa asilimia chache.
Na hii pengine inaweza kuwa chachu ya kuongeza hata vipato vya wakazi wengi wa jiji hili japo kwa asilimia chache.
Na sasa watu
waliowengi wamekuwa na
shahuku kubwa ya
kutaka kujua endapo
kweli mradi huo
wa mabasi
yaendayo kasi, kama
utakuwa ni
suluhisho la kweli
na kamili
la tatizo la
foleni katika jiji
la Dar es
salaam.
Hivyo basi serikali na mamlaka husika inabidi kuhakikisha kuwa , hawawaangushi na itakata kiu kwa wananchi kupitia mradi huo unaoendelea, Na umma wa watanzania unaamini kukamilika kwa ujenzi huo kweli ktakuwa suluhisho la foleni za magari jijini dar es salaam, kwani ni ukweli kwamba macho ya watanzania wote kwa sasa yapo katika kutazama ujenzi huo, na wakazi wa jiji hilo kwasasa wanavumilia adha kubwa wanayoipata ikiwa ni pamoja na foleni kuongezeka mara dufu kutokana na ujenzi huo kuendelea lakini mioyo yao na nafsi zao zikiamini kuwa mwisho wa siku watanufaika na mradi huo..
0 comments:
Post a Comment