Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari
aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za
Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Akizungumza
katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa
bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo
mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.
Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.
"Nimefarijika
sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi
yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na
ndoto yangu,'' alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe
kanisani.
0 comments:
Post a Comment