picha ni moja ya treni inayo fanya kazi ua safirishaji jijini dar picha na maktaba |
Dar es Salaam. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza amekufa papo hapo na mwingine wa kidato cha tatu kujeruhiwa baada ya kugongwa na treni.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Reli Tanzania,
Saada Haji alisema ajali hiyo ilitokea saa 1.30 usiku wa juzi na kwamba
aliyekufa ametambulika kuwa ni Beatrice Olive (14).
Alisema wakati wa uhai wake, Beatrice alikuwa
anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kambangwa,
iliyopo wilayani Kinondoni.
Alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni, Scolastika Kipinda (18) anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mzizima.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukatwa miguu yote.
Alisema wanafunzi hao ambao ni ndugu, walikumbwa na ajali hiyo wakati wakivuka kwenye Daraja la Buguruni kwa Mnyamani.
Kamanda Haji alitangaza kuwa daraja hilo ni la hatari kwa wananchi wanaolitumia kupita kwa miguu
.Chanzo mwananchi
.Chanzo mwananchi
0 comments:
Post a Comment