Ligi
kuu ya Vodacom sasa itarushwa moja kwa moja kupitia Azam TV ili
washabiki wa mpira wa miguu Tanzania waweze kujionea mechi kali za ligi
kuu muda wowote na mahali popote zitakapochezwa. Ligi hizi zitaonyeshwa
katikati na mwisho wa wiki.
Ratiba za mwisho wa wiki hii:
Jumamosi tarehe 25 Januari:
Ashanti United na Young Africans zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
Azam FC na Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Jumapili tarehe 26 Januari:
JKT Ruvu na Mgambo JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Simba SC na Rhino Ranger zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
Ratiba za wiki ijayo:
Jumatano tarehe 29 Januari:
Azam FC na Rhino Rangers JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Coastal Union na Young Africans zitacheza Uwanja wa Mkwakwani (Tanga)
Alhamis Tarehe 30 Januari:
Ruvu Shooting na Mbeya City zitacheza Uwanja wa Mabatini (PWANI)
Mechi zitaonyeshwa moja kwa moja kuanzia saa kumi kamili jioni.
Katika
habari nyingine mpya na za kusisimua, mashabiki sasa watakuwa na uwezo
wakuangalia dondoo za mechi zote kupitia simu zao za mkononi, ikiwapa
fursa ya kuangalia matukio yaliyopita na kujua yatakoyojiri mechi
zijazo.
“Baada
ya kupata kibali cha kuonyesha ligi kuu ya Vodacom, moja kati ya
malengo makuu ni kuhakikisha kuwa tunafikia kiwango cha juu cha
kimataifa. Katika kufanikisha hili, tumewekeza Zaidi kwenye teknolojia
ya kisasa ya matangazo ya nje na mafunzo ya wafanyakazi wetu. Na
tumedhihirisha hilo kwamba tumejizatiti katika kutoa matangazo yenye
ubora wa hali juu tuliporusha Ligi ya kombe la Mapinduzi lililomalizika
hivi karibuni” Amesema Rhys Torrington, mkurugenzi mkuu wa Azam Media.
Azam
Media Ltd waliingia mkataba wa miaka mitatu (3) na TFF wa haki za
kutangaza na kuonyesha mechi zote za ligi kuu ya Vodacom wenye thamani
ya Tshs 5,560,800,000.
AzamTV
tayari inaonyesha chaneli Zaidi ya 50, zinazojumuisha chaneli maarufu
za kimataifa na za kitaifa na chaneli tatu maalumu kutoka Azam. Chaneli
hizo maalum ni:
-Azam One – Burudani motomoto kwako na familia kutoka bara la Afrika, ambazo nyingi ni kwa lugha ya Kiswahili.
-Azam Two – Programu maalum mbalimbali zilizochaguliwa ulimwenguni.
-Sinema Zetu – Chaneli maalumu inayoonyesha filamu za kitanzania masaa 24.
Kwa
ujumla, chaneli hizi zinawapa fursa wateja wetu kuweza kuangalia
kiwango cha juu cha michezo mbalimbali, filamu, vipindi vya watoto,
tamthilia, maisha na burudani na mengineyo kwa bei nafuu kabisa ya Tshs
12,500/= tu!
Kwa
sasa Azam TV inapatakana Tanzania tu, lakini kwa wiki chache zijazo
itaanza kupatikana Uganda na Kenya, kabla ya kuenea Afrika Mashariki kwa
ujumla. Kwa ujumla AzamTV inakupa nafasi yawewe na familia yako kupata
burudani mbalimbali kwa bei rahisi na nafuu.
Azam
Media itaendelea kuwekeza kwenye utengenezaji wa programu mpya za ndani
ya nchi kupitia kampuni tanzu ya Uhai Productions kwa ushirikiano na
watengeneza vipindi wa kitaifa.
0 comments:
Post a Comment