>>WENGER AKANUSHA KUMSAINI JULIAN DRAXLER WA SCHALKE!
KESI YA 'QUENELLE' YA ANELKA KUSIKILIZWA FEBRUARI MWISHONI
Kesi inayomkabili Straika wa West Bromwich, Nicolas Anelka, kwa kutoa
Saluti ya 'quenelle' ambayo inatuhumiwa kama ni ya Kibaguzi itaanza kusikiliwa mwishoni mwa Februari kwa mujibu wa FA.
Anelka amepinga tuhuma hizo na akipatikana na hatia huenda akafungiwa Mechi 5 au zaidi.
Anelka, Miaka 34, alitoa Saluti hiyo
ambayo Mkono mmoja unanyooshwa chini na mwingine kupita Kifuani na
kuugusa mwingine, wakati alipofunga Bao kwenye Mechi na West Ham hapo
Desemba 28 iliyokwenda Sare Bao 3-3.
Anelka alikabidhiwa Kabrasha la Kurasa 34 likielezea Tuhuma dhidi yake.
ESSIEN AENDA AC MILAN
Chelsea imethibitisha kuwa imekubaliana na AC Milan kuhusu Uhamisho wa Michael Essien ambao hauna Dau lolote.
Essien, Miaka 31, ni Mchezaji wa
Kimataifa wa Ghana, na Msimu uliopita alikuwa na Real Madrid kwa Mkopo
na kuhamia kwake AC Milan kutamfanya awe ndie Mchezaji wa kwanza
kusainiwa na Meneja mpya Clarence Seedorf.
Essien alianza kucheza Soka huko Ulaya kwenye Klabu ya Ufaransa Bastia akiwa na Miaka 17.
Mwaka 2003, Essien alijiunga na Lyon na
kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi 1 Mwaka 2005 kabla Mwaka huo
kuhamia Chelsea kwa Dau la Rekodi ya Klabu kwa wakati huo la Pauni
Milioni 24.4 na kuichezea zaidi ya Mechi 250.
WENGER AKANUSHA KUMSAINI JULIAN DRAXLER WA SCHALKE!
Arsene Wenger amezitupilia mbali ripoti kuwa Winga wa Schalke Julian Draxler amesaini Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 37.
Wenger amesema anao Mawinga wengi na hatamsaini Draxler.
Akiongea baada ya Jana kuifunga Coventry
4-0 kwe FA CUP, Wenger alisema: “Hiyo ni dhana tu. Hamna kinachotokea,
hapana, kweli, hapana. Hatuhitaji kusaini Mchezaji wa Wingi. Tunao
Mawinga 17!”
WAYNE ROONEY AKARIBIA KUSAINI MKATABA MPYA OLD TRAFFORD!
Ukisainiwa, Mkataba huu utamweka Old
Trafford hadi 2018 na kuzipiga kibega Klabu za Chelsea, Real Madrid na
Arsenal ambazo zimeripotiwa sana kumwinda.
Habari hii, ambayo imelipuliwa na Gazeti
moja kubwa huko England likidai ni habari za uhakika toka ndani ya
uongozi wa Manchester, zinakuja mara tu baada ya Man United kuthibitisha
kumsaini Juan Mata toka Chelsea.
Rooney, ambae mara mbili ilidaiwa
anataka kuiham Man United na Chelsea kutoa Ofa mbili mwanzoni mwa Msimu
ili kumnunua,inasemekana aliwaamrisha Mawakala wake kuanza kuzungumza na
Uongozi wa Man United mwanzoni mwa Mwezi huu ili kukubaliana Mkataba
mpya utakaobadili huu wa sasa unaomalizika baada Miezi 18 na ambao
unamlipa £250,000 kwa Wiki.
0 comments:
Post a Comment