
Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja
na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa mjini Zanzibar
kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya
CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud Thabit Kombo kuwa
mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa
jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea wa nafasi
uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM.Picha na Adam H. Mzee
0 comments:
Post a Comment