Tuesday, 14 January 2014

HILI NDILO DAMPO JIPYA NA LA KISASA LA KUTUPIA TAKATAKA LINALO JENGWA JIJINI MBEYA.

Huu ndio mwonekano wa Dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwisho za ujenzi  Dampo hilo linajengwa maeneo ya mlima nyoka jijini Mbeya na kazi kubwa pamoja na kuhifadhi takataka pia litatumika kufua umeme na kutengeneza mbolea.

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.
Huu ndio mwonekano wa Dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni 
 Hili ni eneo ambapo magari yaliyobeba takataka yatakua yanaingia na kumwanga taka taka hizo 
 Mwonekano wa Karibu wa ndani wa Dampo hilo la kisasa Jijini Mbeya 
 Hii ni Chemba pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na kupelekwa katika Bwawa maalum litakalo tumika kutengenezea umeme pamoja na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea.
 Hapa Ndipo Takataka hizo zitakuwa zikitelemkia 
 Mwonekano zaidi wa Dampo hilo la kisasa kwa ndani ambapo kwa sasa wameweka kokoto ndogondogo chini  huku ujenzi ukiendelea 
 Kingo pembezoni mwa Dampo hilo la kisasa

Related Posts:

0 comments: