>>CHARLTON 249, ROONEY 208!
Wiki iliyopita kulivuja habari kuwa
Rooney yuko tayari kusaini Mkataba mpya kuendeleza huu wa sasa
unaomalizika mwishoni mwa Msimu ujao na ambao utakuwa ukimlipa Pauni
300,000 kwa Wiki.
Jana Rooney alitamka kuwa anategemea
kuivunja Rekodi ya Ufungaji Magoli ya Manchester United iliyowekwa na
Lejendari Sir Bobby Charlton nah ii ilileta uthibitisho kuwa atasaini
Mkataba mpya.
Rooney alisema: “Siku zote nimesema mie natilia mkazo Soka langu tu na kujaribu kufanya vyema ili Timu iwe na mafanikio!”
Hadi sasa Sir Bobby Charlton ndie Mfungaji Bora wa Man United akiwa na Bao 249 na Rooney amefikisha Bao 208.
Akizungumzia Rekodi hiyo, Rooney alisema: “Kama nitaifikia, nitasikia fahari kubwa kwa sababu ipo kwa muda mrefu!”
Pia zipo fununu kuwa Rooney ndie atakuwa
Nahodha mpya wa Man United baada kuondoka Nemanja Vidic mwishoni mwa
Msimu huu kufuatia kumalizika Mkataba wake.
Wakati huo huo, Man United inatarajiwa
kwenda Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu mara baada ya Mechi yao na
Arsenal hapo Jumatano Usiku kwa Ziara ya Mazoezi.
Baada ya Mechi hiyo na Arsenal, Man united hawana Mechi nyingine hadi baada ya Siku 10 watapoivaa Crystal Palace.
0 comments:
Post a Comment