Wakuu wa Afrika Kusini
wanachunguza kifo cha afisa wa chama cha wafanyakazi kwenye mapambano na
polisi wakati wa mgomo katika mgodi wa dhahabu nyeupe.
Msemaji wa polisi alieleza kuwa mtu huyo
alipigwa risasi na kuuwawa Ijumaa, wakati polisi walipojaribu
kuwatawanya waandamanaji katika barabara inayoelekea kwenye mgodi katika
jimbo la Limpopo, kaskazini mwa nchi.
Lakini alisema hakuna hakika ikiwa mtu huyo alipigwa risasi na polisi au walinzi waliokuwako hapo.
0 comments:
Post a Comment