Waandamanaji nchini Thailand
wanazuia usambazaji wa karatasi za kupigia kura siku moja tu kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaosusiwa na upinzani.
Makundi ya waandamanaji wanaopinga serikali
yalizingira ofisi moja ya serikali katika mji mkuu wa Bangkok ,ambapo
karatasi za kupigia kura katika zaidi ya vituo 100 zimewekwa.Upinzani unataka kuondolewa kwa kile inachokitaja kama serikali fisadi ya waziri mkuu Yingluck shinawatra ambaye wamekuwa wakidai ni kibaraka wa kakaake mkubwa Thaksini Shinawatra.
Thailand inajiandaa kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumapili,licha ya upinzani kuususia na hata kutatiza maandalizi yake. Inaarifiwa huenda bwana Yingluck shinawatra akachaguliwa tena, kitu kinachowaudhi wapinzani.
Mamia ya waandamanaji walipiga kambi katika vituo vya kusambazia karatasi za kupigia kura mjini Bangkok ili kuzuia shughuli ya kusambaza karatasi hizo kabla ya uchaguzi mkuu Jumapili.
Polisi walijitahidi kuwatawanya wafuasi wa serikali na wapinzani baadhi waliokuwa wamejihami kwa vijiti na vyuma huku hali ya taharuki ikitanda mjini Bangkok.
0 comments:
Post a Comment