Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Iringa
Frenck Leonard akiongea na waandishi baada ya kuachiwa na Polisi alipo kamatwa ndani ya mahakama wakimtuhumu kuvunjasheria wakati akisikiliza kesi ya Mshitakiwa wa mauaji ya Daud Mwangosi aliekuwa mwandishi wa Chanel ten na Mwenyekiti wa (IPC).
Waandishi wa habari Wakiwa viwanja vya mahakama ya wilaya iringa wakisubili kupata maelezo kwa msajili wa mahakama juu ya kitendo cha Polisi kumkamata Mwennyekiti wa IPC wakimshuku kuvunja sheria ndani ya mahakama kosa ambalo halikujulikana nakupeleke kumuachia huru.
Askari kanzu wakimpa ulinzi mtakatifu mshitakiwa wa kosa la mauaji ya aliekuwa muandishi wa chanel ten Daudi Mwangosi wakati ana toka mahakamani leo kwa kumpandisha katika gari maalumu ili asipigwe picha na waandishi baada ya kesi yake kuandikishwa rasimi katika mahakama kuu na itajadililiwa katika kikao kitakacho pangwa tayali kwa kusikilizwa.
WAKATI
mahakama kuu kanda ya Iringa jana ikianza kusikiliza kesi ya mauwaji
ya aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten na mwenyekiti wa chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) marehemu Daudi Mwangosi ,polisi
mjini Iringa waanza kuwanyanyasa wanahabari wanaofika kufuatilia
kesi hiyo baada ya kumkamata mwenyekiti wao Frank Leonard akiwa ndani ya
mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea.
Hata
hivyo katika hali iliyowashangaza wananchi na wanahabari
waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo ni baada ya askari
mmoja kusimama ghafla katika kiti chache na kwenda kwa wakili wa
serikali na kurudi eneo ambalo wanahabari walikuwa wamekaa na
kumsimamisha Leonard na kwenda kumpeleka kituo cha polisi kwa madai
kuwa amepiga picha mahakamani hapo wakati jaji akiendelea na kesi
jambo ambalo si la kweli.
Akizungumia
uamuzi huo wa askari hao kumkamata Leonard alisema kuwa aatambua
taratibu zote za kimahakama na kuwa asingeweza kupiga picha wakati
jaji akiendelea na kesi na kuwa kilichotokea baada ya kuingia
mahakamani hapo kamera yake ilikuwa ndani ya mfuko huku yeye
akiendelea kuchukua maelezo kwa kuyaandika .
Hata
hivyo alisema wakati huo simu yake aliyokuwa ameiweka mfukoni
wakati akiitoa mfukoni na kutaka kuiweka vizuri askari huyo aligeuka
na kuona ameishika simu hiyo na hivyo kuhisi kama amepiga picha na
kumkamata na kutaka
kumbambikia kesi ya kupiga picha mahakamani ila baada ya uchunguzi
wa awali na maelezo ilibainika si kweli na ndipo alipoachiwa huru na
kutakiwa kuripoti baada ya muda kituoni hapo.
Kabla
ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo wa IPC wanahabari zaidi ya 10
waliokuwepo mahakamani hapa mapema majira ya saa 2 asubuhi walizuiwa
na askari polisi waliomfikisha mahakamani mtuhumiwa wa mauwaji hayo kuwa
hawapaswi kuingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo
kabla ya kufikisha malalamiko hao kwa msajili wa
mahakama ambae alipinga hatua ya jeshi la polisi kufukuza wanahabari
mahakamani hapo.
Hatua ya polisi hao kumkamata mwanahabari huyo iliwalazimu wanahabari kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Iringa kwa
njia ya simu ili kuhoji uhalali wa jeshi la polisi kuzuia
wanahabari katika mahakama hiyo na kwakesi hiyo ya askari anayetuhumiwa kufanya mauwaji ya Mwangosi.
Akizungumza
kwa njia ya simu akiwa safarini kamanda Mungi alisema polisi hawana
mamlaka ya kuwazuia wananchi ama wanahabari
wanaofika mahakamani kwani mwenye mamlaka ya kufukuza ama kuagiza
kwa mtu yeyote anayevunja sheria ndani ya mahakama kukamatwa ni
hakimu ama jaji anayesikiliza kesi na si polisi .
Hata
hivyo wanahabari hao wameeleza kusikitishwa na askari polisi hao
kuendelea kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari katika kesi hiyo ya
Mwangosi huku kesi nyingine zikiwemo za wana siasa kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma za vurugu polisi
hao wamekuwa wakionyesha urafiki wa
hali ya juu na wanahabari na hata kuwapigia simu ili kufika
mahakamani ila inapofika kesi ya mwenzao huyo wamekuwa wakiwageuka
wanahabari na kuwaona adui .
Mtuhumiwa
huyo ambae alifikishwa mapema zaidi kuliko simu nyingine na gari la
polisi akiwa mbele aliondolewa mahakamani hapo kwa kufishwa kupita
kiasi na
kuingizwa katika gari dogo binafsi lenye namba T
165 BMP lililokuwa likiendeshwa na askari mwanamke (WP) huku vioo vya
gari hilo vikiwa haviangazi kwa ndani huku watuhumiwa wawili wa
mauwaji ambao walikuwa na askari huyo mahakamani hapo wakipakiwa
katika karandinga la polisi.
Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda
ya Iringa, Dunstan
Nduguru aliwashangaa Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama.
"Hata
kama mwandishi huyo angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka
wapewe agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.
Pamoja
na askari hao kuwazuia wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo
kufikishwa mahakamani, Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu
wanahabari kuchukua picha kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza
na baada ya shughuli hizo kwisha.
"Kuwazuia
wanahabari kufanya kazi zao kwa utaratibu huo sio sahihi; siku nyingine mkiona
kuna dalili ya kupata bugudha kama hiyo naomba mnijulishe ili niondoe mzozo
huo," alisema.
Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Mary Shangali, Wakili wa upande wa mashtka, Adolph Maganga alisema Adolph Maganda alisema kwa kukusudia mtuhumiwa Pacificius Cleophace Simoni anatuhumiwa kumuua Mwangosi kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Alisema
katika tukio hilo lililotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo,
wilayani Mufindi mkoani Iringa, mshtakiwa alifyatua bunduki yake na kusababisha
kifo cha marehemu, papo hapo.
Alisema
siku ya tukio marehemu alikuwa Nyororo kwa ajili ya kuripoti na kutoa taarifa
kwa umma juu ya mkutano uliokuwa ufanywe na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema).
Alisema
mshtakiwa akiwa mmoja wa wafanyakazi wa Polisi, waliwasihi Chadema wasifanye
mkutano huo kabla wafuasi wake hawajaanza kurusha mawe kwa Polisi na baadhi yao
kupata majeraha.
Kutokana
na mzozo huo, wakili huyo wa serikali alisema polisi walipiga mabomu ya machozi
ili kuwatawanya wafuasi hao kabla mshtakiwa huyo hajamfyatulia bomu marehemu.
Wakili
huyo aliwasilisha ramani ya eneo la tukio, ripoti ya mtaalamu wa milipuko na
ripoti ya daktari aliyechunguza mwili wa marehemu Mwangosi na gazeti la Mwananchi
la Septemba 3, 2012 lililochapisha picha ya tukio hilo katika
ukurasa wa mbele kama vielelezo vinavyohusiana na kesi hiyo.
Wakili
wa upande wa utetezi Lwezaula Kaijage alitaja mambo wanayokubaliana katika kesi
hiyo kuwa ni jina na anuani ya mshtakiwa na kwamba marehemu Mwangosi alikufa
kifo ambacho si cha kawaida.
Mtuhumiwa huyo wa mauwaji askari wa FFU Pacificus Cleophase Simon aliyekuwa na miaka 23 wakati akitenda kosa hilo alisomewa shitaka hilo la kuua kwa kukusudia na wakili wa serikali Maganga mbele ya jaji Shangali huku upande wa utetezi wakipinga baadhi ya vielelezo kutumika mahakamani hapo kama ushahidi katika kesi hiyo.
Wakili
wa serikali alisema kuwa moja kati ya vielelezo ni pamoja na
taarifa ya kifo cha marehemu Mwangosi
vinavyoonyesha Mwangosi aliuwawa ,pia mshitakiwa
alihojiwa kwa onyo na Nidhamu na katika maelezo yake alikubali kosa
,tatu mtuhumiwa huyo siku ya tukio tarehe 2 septemba 2012 alikubali
kuwepo eneo la Nyololo ambako mauwaji hayo yalifanyika na kusikia mkuu
wa polisi Mafinga Aser Mwampamba akipiga kelele kuwa anapigwa kabla
ya yeye kufika na akiwa na silaha na kufyatua risasi na kumuua
Mwangosi .
Alisema wakili huyo kuwa mtuhumiwa alikiri silaha iliyoonyeshwa katika
gazeti la Mwananchi la Septemba 3 mwaka 2012
kuwa ndio ilitumika kufanya mauwaji hayo
Hata hivyo wakili
wa upande wa utetezi Lwezaula Kaijage ulikubali jina la
mtuhumiwa na anwania yake pia kukubali kuwa Mwangosi kweli alikufa
kwa kifo kisicho cha kawaida na hakuna ubishi kama alikufa Nyololo
pia unakubali kuwa mtuhumiwa alikamatwa ila vingine vyote si sahihi na
kutaka aliyehariri picha katika gazeti la Mwananchi kabla ya gazeti
hilo kutumika kama kielelezo kuitwa na kuhojiwa pia hakuna uvbishi kama mshtakiwa Simoni alikamatwa na amefikishwa mahakamani akihusishwa na
mauaji hayo.
Chanzo, Mnyalublogspot.com Francis godwinblog
0 comments:
Post a Comment