Wednesday, 12 February 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI (WATU SITA WASHIKILIWA KWA KUUA )

DSC00207 
WATU SITA WASHIKILIWANA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUMUUA MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA  JINA  WALA MAKAZI  YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA [06]  KWA MAHOJIANO ZAIDI AMBAO NI 1.FAINES ZIMAMA [65] 2.GIBSON MWAKALIBULE [44] MWENYEKITI WA MTAA WA IBARA 3.EMA MLIGO [46] 4.EMANUEL EDSON [24] 5.VAILETH EDSON [17] NA 6. BAHATI EDSON [20] WOTE WAKAZI WA MTAA WA IBARA UYOLE JIJINI MBEYA BAADA YA  KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA MTU MMOJA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA  KIUME MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 30-35 WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.02.2014 MAJIRA YA  SAA 03:00HRS WAKATI MAREHEMU ALIPOKUTWA AMESIMAMA KATIKA ENEO LA NYUMBANI KWA FAINES ZIMAMA AMBAYE KWA KUSHIRIKIANA NA FAMILIA YAKE WALIPIGA KELELE NA WATU KUTOKA NJE KISHA KUMSHAMBULIA MAREHEMU HADI KUFA. CHANZO BADO KINACHUNGUZWA.  . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA MTU/WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA WATU WA ENEO HILO NA JIJI LA MBEYA KWA JUMLA KUFIKA KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA KWA AJILI YA  UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 16  BAADA YA  KUKAMATWA WAKIWA NA BHANGI KETE 55.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 16 WAKIONGOZWA NA WAMI MGALAH [26] WOTE WAKAZI WA MITAA YA MWAKA NA TUKUYU ENEO LA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA  MBEYA BAADA YA  KUKAMATWA WAKIWA NA BHANGI KETE 55 AMBAZO NI SAWA NA UZITO WA GRAM  275. WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 11.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS MAENEO HAYO KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA KWA USHIRIKIANO KATI YA JESHI LA POLISI TUNDUMA TANZANIA NA JESHI LA POLISI NAKONDE NCHINI ZAMBIA KATIKA MAENEO YA  MPAKA. WATUHUMIWA HAO NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI
JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LAWASHIKILIA WATU  17 RAIA WA NCHINI ETHIOPIA BAADA YA  KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 17  WAKIONGOZWA NA RAMATHO SHUKURANDA [19] WOTE RAIA NA  WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA  KWA KUINGIA NCHINI BILA KUWA NA KIBALI. WATU HAO  WALIKAMATWA TAREHE 11.02.2014 MAJIRA YA  SAA 18:00HRS ENEO LA VWAWA KATIKA BARABARA KUU YA  MBEYA /TUNDUMA WAKIWA KATIKA GARI NDOGO AINA YA  NOAH YENYE NAMBA ZA USAJIRI T.340 BUP LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MTANZANIA LUGANO ALBERT @ MLAWA [25]  MKAZI WA WILAYA YA  KYELA AMBAYE PIA AMEKAMATWA. WATU HAO WALIKAMATWA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA  KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Related Posts:

0 comments: