MTU MMOJA ANAYESADIKIWA KUWA JAMBAZI SUGU AMEUAWA NA WANANCHI WILAYANI MOMBA.
MNAMO TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:20
HRS JIONI MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HEZRON MWAISANILA (22)
MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU
HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA BAADA YA KUSHAMBULIWA
NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA
JADI FIMBO NA MAWE. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA
MAREHEMU HUYO AKIWA NA WENZAKE WAWILI WALIOKIMBIA WALIPORA
FEDHA TASLIMU TSHS. MILIONI 1,200,000/=, ZAMBIA KWACHA MILIONI
1,200,000/=, DOLA ZA KIMAREKANI 60 NA SIMU YA KIGANJANI MALI YA DENIS ODAS (22) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAPOROMOKO – TUNDUMA MAJIRA YA SAA 16:45HRS JIONI AKIWA
ANATOKA DUKANI. MAREHEMU ALIKUWA NI JAMBAZI SUGU NA ALIKUWA ANATAFUTWA
NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU LIKIWEMO TUKIO LA
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA BAADA YA KUPORA PESA NA GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA TOYOTA KLUGER MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA AKITUMIA SILAHA AINA YA SMG NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA AITWAYE OBADIA JANAS (41) MKAZI WA ISYESYE KWA KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WA UHALIFU
WANAOWAKAMA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI
ZA KISHERIA.
WATU 07 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI MBUNGE.
MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI – CCM MHE. JACKSON MWANJALI (55)
ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RUNGU NA FIMBO KICHWANI NA KUNDI LA VIJANA
WANAODAIWA KUWA NI WAFUASI WA CHADEMA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE
09.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SHIPONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MBUNGE HUYO AKIWA NA SHADRACK MWATUNGUJA -
KATIBU WA UCHUMI NA MIPANGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA BAADHI YA
VIONGOZI WA CCM WA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKIWA WANATEMBELEA VITUO
VYA KUPIGIA KURA KATIKA KATA YA SANTILYA AMBAVYO VIPO KATIKA JIMBO LAKE.
MTUHUMIWA PAUL WUMBULA (32) MKAZI WA MBALIZI NA WENZAKE SITA
WALIKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. WAHANGA WALIPATIWA MATIBABU NA
KURUHUSIWA, HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA VURUGU KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA KUMCHUKULIA HATUA ZA
KISHERIA MTU YEYOTE YULE ATAKAYEJIHUSISHA NA KITENDO CHOCHOTE CHA
UVUNJIFU WA AMANI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment