Wednesday, 12 February 2014

SHULE YA MAKETE GIRLS YAMKUNA MKUU WA MKOA WA NJOMBE

 
IMG_3304
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi (katikati) akikagua majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
IMG_3306
Ukaguzi huo ukiendelea.
IMG_3307
 Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao.
IMG_3308
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo.
IMG_3310
Kamati Kuu yateua mgombea wa CCM Kalenga Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
====
Kufuatia kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika
Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea wanafunzi
Akizungumza na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari
“Ndugu zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu” alisema Msangi
Katika hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Shule hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi pamoja na wadau mbalimbali

habari/picha na Edwin Moshi, Makete.

Related Posts:

0 comments: