Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari
Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga(mbele aliyesimama) akiongea na Maafisa
Habari na Mawasiliano kuhusu ushirikiano wa serikali na vyombo vya
Habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini.Wakati wa Mkutano wa
Mwaka wa Maafisa Habari na Mawasiliano leo Mkoani Tanga.
Baraza la Habari Tanzania limesema
kuna haja ya kujenga miundombinu itakayoboresha ushirikiano kati ya
Maafisa Habari na Vyombo vya Habari ili kuboresha utendaji kazi katika
tasnia ya habari.
Akizungumza katika kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachoendelea mjini Tanga, Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga amesema ili sekta ya habari iweze kuboreka ni lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari.
Anasema kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kufanya kazi kwa pomoja kutokana na ukweli kwamba kila upande unamhitaji mwenzake ili kutimiza majukumu yake.
"kimsingi tunahukumiwa kufanya kazi kwa pamoja" alisema Bwana Kajubi, akinukuu sehemu ya Hotuba aliyotoa Mhe. Rais Jakaya mrisho Kikwete katika moja ya mikutano ya "open Government uliofanyika London Uingereza.
Akizungumza kuhusu fikra mgando katika Vyombo vya Habari, anasema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wanahabari kugeuka kuwa wanaharakati na kuvaa fikra ya kupambana na serikali kama wanavyofanya wanaharakati.
"Kama habari nzuri za serikali haziuzi mbona Timu ya Taifa au Mwakilishi wa Taifa kwenye mashindano ya Kimataifa akishinda watu hupenda kusoma" Anasema Bwana Kajubi.
Anasema kwa maoni yake kushikilia kuandika matatizo tu kuhusu nchi yetu sio kuisaidia nchi na hakujengi moyo wa wananchi kujiamini na uzalendo.
Bw. Kajubi alikuwa akitoa mada kuhusu Ushirikiano wa serikali na Vyombo vya habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini katika kikao kazi za Maafisa Habari na Mawasiliano. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano unawahusisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Serikali za Mitaa, Mikoa na mashirika ya umma wapatao 130 kutoka nchi nzima. Chanzo: Assah Mwambene

0 comments:
Post a Comment