Monday, 10 February 2014

LA LIGA: MESSI BAO 2, BARCA YARUDI KILELENI!

>>JUMANNE NI MARUDIANO NUSU FAINALI COPA del REY!!
MESSI_ASHANGILIA_GOLIMABINGWA wa La Liga huko Spain, Barcelona, Jana walirudi kileleni mwa Ligi hiyo baada ya kuifunga Sevilla Bao 4-1 huku Supastaa wao, Lionel Messi, akipachika Bao mbili.
Barca wako juu wakifungana kwa Pointi na Real Madrid na Atletico, zote zikiwa na Pointi 57 kila mmoja, lakini Barca wako mbele kwa ubora Magoli.
Kwenye Mechi hiyo Sevilla walitangulia kufunga kwenye Dakika ya 15 kupitia Alberto Moreno na Barca kusawazisha Dakika ya 34 Mfungaji akiwa Alexis Sanchez na kisha Messi kupiga Bao 2 katika Dakika za 44 na 56.
Fabregas ndie alieifungia Barca Bao la 4.
Kesho Jumanne Usiku, Spain itakuwa na Mechi za Marudiano za Nusu Fainali za Copa del Rey kwa Atletico kucheza na Real na Barca kuwa Ugenini kwa Real Sociedad.

MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
FC Barcelona
23
18
3
2
63
17
46
57
2
Real Madrid CF
23
18
3
2
65
24
41
57
3
Atletico de Madrid
23
18
3
2
56
16
40
57
4
Athletic de Bilbao
22
13
4
5
42
28
14
43

COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [0-3] [Estadio Vicente Calderon]
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2] [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19

Related Posts:

0 comments: