>>DAKTARI MKUU FIFA AONYA: “TUTAKUJA WAKATI WOWOTE, MAHALI POPOTE!”
FIFA wanataka Timu zote 32
zitakazoshiriki Fainali hizo za Brazil kutuma Ratiba yao ya wapi Timu
zao zitakuwepo kabla Machi 1 kwao ili waweze kujua wakati gani Wachezaji
hao watapimwa.
Hata hivyo, Jiri Dvorak ameeleza
Wachezaji hao na Timu zao hawatajua ni wakati gani Wapimaji watatua
Kambini mwao na watahakikisha kuwa hakuna Timu itakayokwepa kupimwa
kabla ya Mechi ya Ufunguzi kati ya Wenyeji Brazil na Croatia hapo Juni
12.
Dvorak amesema: “Nina furaha kuwa Watu
wana wasiwasi udhibiti wa Madawa Marufuku utaanza lini kwa sababu
hatutangaza. Tutakuja wakati wowote, mahali popote!”
Aliongeza: “Kuanzia Machi 1, tutaomba
tujue Ratiba ya Timu zitakuwa wapi. Na sisi Makao Makuu tutaamua wakati
gani tutazifuata. Kwa kuweka wazi, tutawapima Wachezaji wote si chini ya
mara moja kabla ya Mechi ya Kwanza!”
0 comments:
Post a Comment