Jumamosi Februari 1
[SAA za Bongo]
[Cape Town Stadium]
1800 MSHINDI WA 3
Zimbabwe v Nigeria
2100 FAINALI
Libya v Ghana
HUKO Afrika Kusini Mjini Cape Town,
Ghana na Libya zitakumbana kwenye Fainali ya CHAN 2014 ambayo ni
Mashindano ya CAF ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani za
Nchi zao tu.
Kabla ya Fainali hiyo kwenye Uwanja wa Cape Town itachezwa Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu kati ya Zimbabwe na Nigeria.
Kwenye Fainali, hii itakuwa mara ya tatu
kwa Ghana na Libya kupambana kwenye michuano hii na mara ya kwanza
ilikuwa Mwaka 2009 kwenye Kundi B na Mwaka huu walikuwa pamoja Kundi C
na katika Mechi zote hizo matokeo ni Sare ya 1-1.
NJIA KWENDA FAINALI:
GHANA
-Kundi C:
Ghana 1 Congo 0
Ghana 1 Libya 1
Ghana 1 Ethiopia 0
-Robo Fainali
Ghana 1 Congo DR 0
-Nusu Fainali:
Ghana 0 Nigeria 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Ghana yashinda Penati 4-1]
LIBYA
-Kundi C:
Libya 2 Ethiopia 0
Libya 1 Ghana 1
Libya 2 Congo 2
-Robo Fainali:
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
-Nusu Fainali:
Zimbabwe 0 Libya 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 5-4]
Ghana na Libya ndio Timu pekee kwenye
michuano ya safari hii huko Afrika Kusini ambazo hazijaonja kipigo na
zote zimetinga Fainali hii kupitia Mikwaju ya Penati kwenye Nusu Fainali
zao ambazo zote zilitoka 0-0.
Kwenye Nusu Fainali, Ghana iliitoa Nigeria kwa Penati 4-1 na Libya kuibwaga Zimbabwe Penati 5-4.
Wakati Libya ina Kikosi chao kamili,
Ghana itakuwa na upungufu kwa kumkosa Beki wao Kwabena Adusei ambae
alitolewa kwa Kadi Nyekundu walipocheza na Nigeria na pia upo wasiwasi
wa kumkosa Straika Yahaya Mohammed alieumia Goti kwenye Mechi hiyo hiyo.
0 comments:
Post a Comment