Bill
Clinton rais zamani wa Marekani aliwahi kuingia kwenye kashfa kubwa ya
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Monica Lewinsky ambaye alikuwa na
miaka 22 kipindi hicho akifanya kazi kama intern ndani ya White house.
Skendo hiyo ilivyoendelea kuwa kubwa ilimpelekea hadi Bill Clinton
kukanusha waziwazi kwa kusema kwamba hakuwa na mahusiano ya kimapenzi na
miss Lewinsky kama ilivyokuwa inasemekana.
Kitu kipya ni kwamba mtandao mmoja huko
Marekani ambao hutoa habari za kuaminika, umetoa habari na kusema kwamba
Bill Clinton alicheza faulo nje ya ndoa yake na actress/model Elizabeth
Hurley.
Ripoti ya mtandao huo unasema kwamba Bill
Clinton alikuwa na uhusiano na model huyo kwa muda wa zaidi ya mwaka
mzima bila mke wake Hillary Clinton kujua.
Ripoti hizi kama zikithibishwa ukweli ndani yake, zinaweza kuharibu
harakati za Hillary Clinton ambaye anajiandaa kugombania urais mwaka
2016.
0 comments:
Post a Comment