Thursday, 2 January 2014

ZITTO AFIKI MAHAKAMA KUU KUZUIA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA KUMJADILI

Leo Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe pamoja na wakili wake Albert Msando, wallifika katika Mahakama kuu jijini Dar es Salaam kutaka mahakama hiyo izuie jina lake lisijadiliwe katika Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kinachotarajiwa kufanyika hapo kesho, Ijumaa, Januari 3 jijini Dar es Salaam.
ZITTO ZUBERI KABWE

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu na Wakili wa CHADEMA, Peter Kibatala nao walifika mahakamani hapo.

Taarifa kutoka mahakamani hapo zinazema kuwa Mahakama Kuu hiyo imekubaliana na ombi la kutokujadiliwa kwa namna yoyote kwenye kikao kwenye kikao hicho hadi rufaa yake ya kupinga Baraza Kuu la chama hicho kuengua nafasi yake ya Unaibu Katibu Mkuu wa Chama hicho itakaposikilizwa.
 

0 comments: