Thursday, 2 January 2014

UCHUNGUZI WA AFRIKA KUSINI KUSIANA NA KIFO CHA PATRICK KAREGEYA

 
Picture
 
—  Aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa Rwanda katika miaka ya 1994 hadi 2004, Patrick Karegeya amekutwa amefariki usiku wa jana jumatano nchini Afrika Kusini.

Mwili wake ulikutwa katika chumba cha moja ya hoteli kubwa za mjini Johannesburg. Kigogo huyo wa zamani wa Rwanda alikua, toka mwaka 2007 kukimbilia ukimbizini na kuwa mpinzani mkuu wa utawala wa Rwanda, awali alikua mshirika wa karibu na rafiki fika wa rais Paul Kagame. Chama chake RNC, kinatuhumu utawala wa Kigali kuhusika na kifo chake.

Mwili wa Patrick Karegeya umekutwa ndani ya moja ya vyumba vya hoteli ghali iitwayo Mihaelangelo, ambayo pia ina ulinzi mkali sana jijini Johannesburg huko nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa polisi nchini Afrika Kusini, vipimo vya macho baada ya kuuwawa, vimeanzishwa ili kujua waliyohusika na kifo chake.

Awali vyanzo vya habari vilifahamisha kwamba Patrick Karegeya alinyongwa. Shingo ya mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi 

wa Rwanda ilikua na uvimbe na kamba iliokotwa kwenye eneo la tukio.

“Alikodi chumba tarehe 29 mwezi disemba, lakini asubuhi ya leo,  Alhamisi polisi ilikuta muili wake umelazwa kwenye  kitanda. Uchunguzi wa kwanza unaonyesha kua shingo yake ilinyongwa, na kumeokotwa ndani ya chumba alichokua alikodi kamba na fulana ambayo ilikua na damu, ikimaanisha kua amenyongwa”, amsema Katlego Mogale, msemaji wa polisi nchini Afrika Kusini, akibaini kwamba vipimo hivyo vitaonesha ni muda gani kifo chake kilitokea.

Katlego Mogale, amesema wameanza kufanya uchunguzi wa kujua kwa nini alijielekeza kwa hio hoteli, na watu wangapi walikua ndani ya ya chumba chake.

“Timu ya wachunguzi inatathmini kwa sasa picha zilizorekodiwa na kamera za ulinzi”, amesema Katlego Mogale.

Mchana wa tarehe 31 Desemba, Patrick Karegeya alimfahamisha mmoja kati ya watu waliyokutana nae kwamba atapashwa kumuona kwa mazungumzo baadaye rafiki yake wa muda mrefu.

Baadaye aliwafahamisha jamaa zake kwamba ana ahadi na rafiki yake wa muda mrefu, ambae anajulikana kwa jina Apollo Ismael Kiririsi, jioni kwenye hoteli Michelangelo Towers.

Jamaa zake waliwasiliana naye mara ya mwisho saa moja na nusu usiku, na toka muda huo, mawasiliano kati ya mkuu huyo wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Rwanda na jamaa zake yalikosekana.

Jamaa na marafiki wa Patrick Karegeya nao pia wanautuhumu utawala wa Rwanda kuhusika na kifo hicho.

Awali mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, Jenerali Kayumba Nyamwasa aliye ukimbizini nchini Afrika Kusini, ambaye pia alinusurika kuuwawa katika mazingira kama hayo mwaka 2010, amesema kwamba ni mauwaji ya kisiasa.

“Sina shaka na tukio hili, serikali ya Rwanda inahusika na kifo cha Patrick Karegeya. Marehemu hakua na ugomvi na mtu yeyote hapa Afrika Kusini, isipokua rais Paul Kagame , ambaye alimfuatila ili amuangamize kwa kipindi chote hiki cha miaka kumi iliyopita. Haya ni mauwaji ya kisiasa, kama jinsi serikali ya Rwanda imekua ikifanya kwa wapinzani wake”, amesema Jenerali Kayumba Nyamwasa.

Patrick Karegeya aliwahi kumshutumu Rais Paul Kagame kwamba alipanga njama ya kuilipua ndege aliyokuemo mtangulizi wake, Rais Juvenal Habyarimana, akilaumu kwamba, Paul Kagame ndiye mwanzilishi wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Duru za Kidiplomasia kutoka Rwanda zinafahamisha kwamba Serikali ya Rwanda haijatoa tangazo lolote linalohusiana na kifo hicho, kwani kesi hio iko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Afrika Kusini.
 
Imenukuliwa kutoka RFI Kiswahili
Source:
http://www.wavuti.com

0 comments: