![]() |
RPC -MUNGI |
MWANDISHI ,DIANA
BISANGAO WA IRINGA
JESHI
la polisi mkoani Iringa linawashikirilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti
likiwemo la Ditrick Swadiko (18) mkazi wa Ndiuka kata ya Ruaha kumbaka mtoto wa miaka 4.
Akizungumza
na mtandao huu
ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 20 januari majira ya
saa 4 na nusu usiku.
Mungi
alisema mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto Khadija ambaye ni mwanafunzi wa awali
katika shule ya msingi Ndiuka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Na
katika tukio jingine, Askari polisi wakiwa doria eneo la Mlandege walimkamata
Isaya Kimota (27) mfanyabiashara na mkazi wa Ipogoro manispaa ya Iringa kwa kosa la kukutwa
na bangi.
Kamanda
Mungi alisema tukio hilo lilitokea tarehe 20 januari majira ya saa 5 kamili
usiku ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na bangi gramu 200 aliyokuwa ameihifadhi
katika bahasha ya kaki.
0 comments:
Post a Comment