UTAPELI wa
kutumia majina ya viongozi
wa ngazi za juu serikali umeendelea
kuchukua kasi hapa nchini baada ya
mwanamke mmoja mfanyabiashara
mjini Iringa kuponea katika tundu
la sindano kutapeliwa kiasi cha Tsh
800,000 na mtu aliyejifanya ni dereva wa
waziri wan chi ofisi ya waziri
mkuu sera na uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi .
Akizungumza na
mtandao huu wa matukiodaima.com
mfanyabiashara Janeth Mbalazi
amesema kuwa tukio
hilo limetokea asubuhi ya leo .
Amesema awali mtu
huyo ambae alijitambulisha kwa
jina moja la Mlelwa alifika dukani hapo majira ya saa 5 asubuhi akiulizia
huduma ya M-Pesa na baada ya kuelezwa
kuwa huduma hiyo ipo ghafla alianza kujieleza kuwa yeye ni dereva wa mbunge wa
jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ametokea Isimani ambapo gari limeharibika
hivyo simu yake ilipotea na
kuomba namba ya mwanamke huyo ili aweze kuituma kwa boss
wake (Lukuvi) ili atumiwe pesa.
“ Nilikubali kumpa namba yangu na hapo
hapo aliituma kwa
boss wake na
kuniuliza jina nikamwambia naitwa
Jeneth na yeye akamueleza boss wake kuwa mimi naitwa Janeth ….baada
ya hapo aliniambia kuwa atatumiwa kiasi cha Tsh 260,000 na kuondoka
eneo hilo”alisema Janeth
Kuwa baada ya dakika kama
30 ilipigwa simu kwa namba ngeni
na kueleza kuwa
amepata namba hiyo kwa dereva
wake na hivyo atatuma kiasi
cha Tsh 400,000 si muda mrefu kwa
madai ni fedha kwa ajili ya dereva
huyo.
“ Nilimuuliza kuwa
kwanini atume 400,000 wakati dereva wake
amesema anataka kiasi cha Tsh 260,000 alidai kuwa kuna tatizo
jingine limeongezeka na kuwa yeye
kwa sasa yupo katika kikao akitoka
atatuma ..japo baada ya muda dereva wake alipiga kuwa uliyekuwa ukiongea nae ni waziri Lukuvi “
Hata hivyo haukupita
muda kama dakika 10 hivi akapiga simu
Mlelwa ambae anadai ni dereva wa Lukuvi na kuuliza kama boss wake amepiga
simu na baada ya kujibiwa kuwa
amepiga bado alimtaka mwamamke huyo
kumpigia simu Lukuvi ili kumueleza kuwa aongeze pesa atume Tsh 800,000
jambo ambalo lilikuwa zito kwake kumpigia Lukuvi isipo kuwa
alimtaka dereva huyo feki ndie afanye kazi hiyo ya kupiga
simu.
“ Sikuweza kukubali
kumpigia simu nilimtaka apige simu mwenyewe
sio mimi ila nilipojaribu kutuma
fedha zaidi ya salio langu ili kujua
jina linalotumiwa katika
namba 0767 946751 hiyo ya mtu anayejiita ni
Lukuvi kweli jina lilikuja Wiliam Lukuvi “
Pia alisema kuwa
tapeli huyo anajiita ni dereva wa Lukuvi namba
yake ni hii 0768990282 na kuwa
baada ya muda alipiga simu na
kuuliza kama ametuma pesa ila nilipomueleza kuwa hajatuma alisema anaomba nimtumie yangu kiasi cha Tsh 300,000 kwa madai kuwa
amepata kifaa eneo la Isimani hivyo
anataka kwenda kufuata na pindi Lukuvi akituma pesa atakata pesa yake na
kumrushia Tsh 500,000 itakayobaki kati ya 800,000 aliziomba kutumiwa na Lukuvi.
“ Ujue nilijiuliza hivi kweli Lukuvi anaweza kutumia
njia hii kutaka pesa wakati
yeye ni kiongozi mkubwa hapa nchini na
pili Lukuvi Iringa ni nyumbani kwake iweje dereva aje katika maduka ya
M-Pesa na asiende kwa katibu wake ama
kwa viongozi wenzake hapa mkoani “
Pona ya dada huyo ni kutaka kujiuliza kwa mwandishi wa mtandao huu kama ananamba ya Lukuvi na
kusimulia mkasa huo na ndipo sura
ya utapeli ilipoonekana na kuweka
mtego kuwa aje achukue Tsh 250,000 ambazo zipo kwanza huku polisi
wakiwa wameandaliwa tayari kwa
ajili ya kumnasa tapeli huyo ambaye hata hivyo hakuweza kutokea zaidi
ya kupiga simu na kuomba kutumiwa kwa M-Pesa jambo mwanamke huyo hakufanya hivyo.
Mwandishi wa mtandao huu
alijaribu kumpigia tapeli huyo bila mafanikio ila baada ya
kufanya uchunguzi kupitia namba
yake ilionyesha kuwa tapeli huyo
anaitwa Faustin Mlelwa .
Akizunzumza kwa njia ya
simu waziri Lukuvi baada ya kupigiwa na mtandao huu alidai kuwa si kweli
kama kuna dereva wake Iringa kwa leo na kuwa
yeye yupo Dar es salaam na kuwa mtu huyo ni tapeli ambae amekuwa
akifanya hivyo katika maeneo mbali mbali
na kusema kuwa kwa upande wake hawezi
hata siku moja kutumia njia hiyo
.
Hata hivyo
aliwataka watanzania kuwa macho na
watu hao ambao wameendelea kuongezeka kwa kutapeli kwa
kutumia majina ya viongozi hapa nchini .
Baadhi ya vijana
wanaofanya kazi katika vijiwe na maduka
ya M-Pesa ,Tigo Pesa na mitando mingine
wamekuwa wakitapeliwa sana
kupitia majina na viongozi wakubwa na
kuwa baadhi wamekuwa wakitapeli kupitia
jina la mtoto wa rais Jakaya Kikwete ,mkuu
wa mkoa wa Iringa , wakuu wa wilaya na baadhi
wanatumia majina ya watu maarufu wakiwemo wanahabari na kuwa tayari wamelizwa sana
Kamanda wa
polisi mkoa wa Ramadhan Mungi amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuchukua tahadhari
dhidi ya watu hao na kuwa pale mtu
anapotumia mbinu kama hizo wasisite kuripoti polisi ili kuchukuliwa hatua kali.
......
|
0 comments:
Post a Comment