Thursday, 23 January 2014

UGUNDUZI WA GESI NA MAFUTA WAFUTA MATAIFA YA MBALI KUTAFUTA FURSA ZA KUWEKEZA NCHINI

 
Naibu Waziri wa Madini Mh. Steven Masele akizungumza na baadhi ya wekezaji waliofika ofisini kwake.DSC_2769 
………………………………………………………………………………………..
Kutokana na ugunduzi wa gesi asilia na mafuta nchini, Tanzania imeonekana kuwa na thamani kwa nchi mbalimbali duniani na  kuiangalia nchi hii kwa namna tofauti na ilivyokuwa awali kwani sasa imeonekana kuwa na utajiri mkubwa.
Ugunduzi huu umepelekea Wizara ya Nishati na Madini kupokea wageni wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika ili kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara baina ya nchi husika.
Hivi karibuni wizara ya  Nishati na Madini imetembelewa na ujumbe toka Jamuri ya Czech nchi ndogo miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika kwa lengo la kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Ujumbe huu uliongonzwa na  Bw. Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya Nchi ya Czech aliyeelezea uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na madini na kusema kwamba awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa maji, gesi  pamoja na nishati jadidifu, na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.
Dub alieleza kuwa maendeleo si tu kutegemea utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia bali inatakiwa nchi ifanye nguvu ya ziada katika kuongeza thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu kwa kujenga viwanda jambo lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.
Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka Wizara  kuelimisha watanzania katika chuo cha madini katika nchi hiyo na kwamba mawasiliano yataendelea kufanyika ili kufikia malengo ya uhusiano huo.
Kwa upande wake Masele amesema kwamba zipo fursa nyingi  za uwekezaji nchini katika sekta ya madini  na zaidi madini ya viwandani lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia ugunduzi wa gesi na mafuta vitalu vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech kuomba vitalu hivyo ili kuweza kushiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi.

0 comments: